Monday, November 3, 2014

KUITWA KWENYE USAILI - Koplo na Konstebo wa Uhamiaji - 11/3/2014



KUITWA KWENYE USAILI - Koplo na Konstebo wa Uhamiaji - 11/3/2014
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
TANGAZO KUITWA KWENYE USAILI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi anapenda kuwatangazia Watanzania walioomba kazi ya Koplo na Konstebo wa Uhamiaji kuwa wanaitwa kwenye usaili utakaofanyika kuanzia 10 Novemba, 2014 hadi tarehe 15 Novemba, 2014. Usaili huu utafanyika katika vituo viwili ambavyo ni Dar es salaam na Zanzibar kwa utaratibu ufuatao:
1. Kwa waombaji wa nafasi 28 (14 za Koplo na 14 za Konstebo) maalum kwa ajili ya Zanzibar watafanyia usaili wao kwenye ukumbi wa Ofisi za Uhamiaji zilizopo Kilimani - Zanzibar kwa tarehe na muda kama ilivyoonyeshwa kwenye orodha.
2. Kwa waombaji wa nafasi 200 (100 za Koplo na 100 za Konstebo) kwa ajili ya Tanzania Bara na Zanzibar, watafanyia usaili wao kwenye kumbi za Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu (DUCE) kilichopo Chang'ombe, Temeke - Dar es salaam kwa tarehe na muda kama ilivyoonyeshwa kwenye orodha.

3. Wasailiwa wote wanatakiwa kufika kwenye vituo vyao vya usaili kabla ya saa 1:30 asubuhi kwa tarehe waliyopangiwa wakiwa na vitu vifuatavyo:-
•Vyeti halisi (original) vya kumaliza na kufaulu masomo (Leaving and Academic Certificates) pamoja na vile vya mafunzo. Matokeo ya muda (result slips) hazitakubalika.
•Cheti halisi (original) cha kuzaliwa pamoja na,
•Picha mbili za rangi (passport-size) Aidha, wasailiwa watapaswa kujilipia gharama zote wenyewe ikiwa ni pamoja na usafiri na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Waombaji wa kazi ambao majina yao hayamo katika orodha hiyo wafahamu kuwa hawakukidhi vigezo. Atakayeona tangazo hili amtaarifu na mwenzake. Tangazo hili linapatikana pia kwenye mbao za matangazo zilizopo kwenye Ofisi zote za Mikoa za Uhamiaji Tanzania.


0 comments:

Post a Comment