Friday, November 7, 2014

AJIRA HALMASHAURI YA MJI WA BABATI - NOV 2014



AJIRA HALMASHAURI YA MJI WA BABATI - NOV 2014
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, anawatangazia wananchi wote wenye sifa, nafasi za kazi kama ifuatavyo:-

KATIBU MUHSUSI DARALA LA III (PERSONAL SECRETARY III) TANO NGAZI YA MSHAHARA TGSB.

SIFA ZA MWOMBAlI:

Awe na Elimu ya Kidato cha nne au sita.
Awe amehitimu mafunzo ya Uhazili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kufaulu mtihani hatua ya tatu.
Awe amepata mafunzo ya Komputa kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika Programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher

Record Management Assistant II ( X 5)
NGAZI YA MSHAHARA TGS C

SIFA ZA MWOMBAlI:
Awe na Elimu ya Kidato cha nne au sita.
Awe amehitimu mafunzo ya Utunzaji wa Kumbukumbu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika ngazi ya Stashahada (Diploma) katika fani ya Masijala.
Awe amepata mafunzo ya Komputa -Windows, Microsoft Office, n.k kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali

Assistant Librarian 
NGAZI YA MSHAHARA TGS B

SIFA ZA MWOMBAlI:
Awe na Elimu ya Kidato cha nne au sita.
Awe amefaulu mafunzo ya Wasaidizi wa Maktaba (National Liabrary Assistant :
Certificate Course) yatolewayo na Bodi ya .
Huduma za Maktaba Tanzania au Cheti kinacholingana na hicho

Artisan ( Land) II-Fundi sanifu ardhi (x 3)
SIFA ZA MWOMBAlI:

Awe na Elimu ya Kidato cha nne au sita.
Awe amehitimu Stashahada ya kawaida katika fani ya Upimaji na Ramani, usimamizi wa Ardhi na Uthamini kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali

Artisan( Water) II -Fundi sanifu maji (x 3)
NGAZI YA MSHAHARA TGS C

SIFA ZA MWOMBAlI:

Awe amehitimu elimu ya Kidato cha nne au cha sita.
Awe amehitimu chuo cha ufundi
kinachotambuliwa na Serikali ana cheti cha ufundi (F. T. C)

Artisan( construction) II ( X 3)
SIFA ZA MWOMBAlI:
Awe amehitimu elimu ya Kidato cha nne au cha Sita.
Awe amefunzu katika Stashahada ya kawaida katika fani za ufundi wa ujenzi kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali

Community development officer II ( X 15)
NGAZI YA. MSHAHARA TGS B

SIFA ZA MWOMBAlI:
Awe na Elimu ya Kidato cha nne au sita.
Awe na Stashahada ya Maendeleo ya Jamii kutoka Vyuo vya Maendeleo ya Jamii (Buhare au Rungemba au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali

WARD EXECUTIVE OFFICER II ( Afisa mitaa) ( X 15)
 NGAZI YA MSHAHARA TGSC

Awe na Elimu ya Kidato cha nne au sita.
Awe amehitimu mafunzo ya Stashahada (Diploma) katika moja ya fani zifuatazo: -Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayasi ya Jamii kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali

APPLICATION INSTRUCTIONS:

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA:
Mwombaji awe Raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote kwenye Halmashauri ya Mji wa Babati.
Barua za maombi ziambatanishwe na nakala za vyeti vya elimu, Taaluma, Cheti cha kuzaliwa na picha mbili za rangi (Passport size)
Barua za maombi ziambatanishwe na maelezo Binafsi ya mwombaji (CV).
Waombaji waliosoma nje ya nchi, waambatanishe uthibitisho wa vyeti vyao kutoka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni saa 9:30 Alasiri.
Waombaji wote wanatakiwa wawe na umri usiozidi miaka 45.
Maombi vote yatumwe kwa anwani ifuatayo:

Mkurugenzi wa Mji, Halmashauri ya Mji,
S. L. P. 383,
BABATI.


Related Posts:

0 comments:

Post a Comment