Thursday, October 16, 2014

NAFASI ZA KAZI UTUMISHI - Oktoba, 2014



NAFASI ZA KAZI UTUMISHI - Oktoba, 2014
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/H/11 16 Oktoba, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza Nafasi za kazi 21 kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira.

1.1 AFISA KAZI II ( LABOUR OFFICER II) – NAFASI 21
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Kazi na Ajira
1.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kupokea na kuchambua malalamiko mbalimbali yanayohusu Sheria za kazi
· Kufanya Ukaguzi wa Utekelezaji wa Sheria za Kazi.
· Kukusanya taarifa na takwimu za kazi kutoka sehemu za kazi.
· Kupokea na kuchambua taarifa za migogoro ya kazi.
· Kupokea na kuchambua maombi ya kuandikisha mikataba ya hiari.
· Kupokea na kuchambua madai ya fidia na kiinua mgongo
· Kuandikisha watafuta kazi (job Seekers)
· Kupokea na kuandikisha nafasi za kazi toka kwa waajiri.
· Kupokea na kuchambua maombi ya vibali vya ajira ya wageni na kutunza
kumbukumbu za ajira za wageni nchini
· Kukusanya taarifa na takwimu zinazohitajika kwa ajili ya kamusi ya Kazi
(Dictionary of Occupational Titles )
1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada ya Sheria au Sayansi ya Jamii (Sociology)
1.1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
i. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
ii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iii. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vyakidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
2kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho
hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi. Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuombaisipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 31 Oktoba, 2014
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
SLP.63100.
Dar es Salaam.


0 comments:

Post a Comment