Wednesday, October 8, 2014

Kuitwa kwenye Usaili Shirika la Viwango Tanzania - 10/8/2014



Kuitwa kwenye Usaili Shirika la Viwango Tanzania - 10/8/2014 Shirika la Viwango Tanzania linapenda kuwatangazia waombaji kazi waliofanya usaili wa awali na kufaulu katika nafasi za Senior Marketing Officer II, Quality Assurance Officer II, Standards Officer II, Metrologist II, Laboratory Technician II, Laboratory Assistant II, Maintenance Engineer II, Human Resource Officer II, Driver II, Personal Secretary II, Assistant Accountant II, Accounts Technician II, Records Management Assistant I, Records Management Assistant II, Librarian II, Assistant Internal Auditor II, Computer System Technician I, Legal Officer II, Editor II, Corporate and Public Affairs Officer II, Maintenance Technician II, kuwa wanaitwa kufanya usaili wa mahojiano ya ana kwa ana kuanzia tarehe 13.10.2014 mpaka tarehe 16.10.2014 katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Viwango Tanzania, Ubungo, Dar es Salaam.

Aidha, waombaji wa nafasi za udereva na Katibu Muhtasi watafanya usaili wa vitendo (practical) tarehe 11.10.2014. saa 3 asubuhi TBS.

Wasailiwa wanashauriwa kuzingatia yafuatayo:

1. Kuja na vyeti halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne na vyeti vya Taaluma ambayo mtahiniwa aliomba.

2. Mtahiniwa atakaye shindwa kuja na vyeti Halisi atakuwa amejiondoa katika usaili.

3. "Provisional Results", "Statement of results", hati za matokeo ya kidato cha nne na sita HAVITAKUBALIWA.

4. Kila msailiwa aje na kitambulisho kinachomtambulisha.

5. Kila msailiwa atajigharimia kwa chakula, usafiri na malazi.

6. Kila msailiwa azingatie tarehe,muda na eneo alilopangiwa kufanya usaili.

7. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa.

Limetolewa na:

Kaimu Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania,
Makutano ya Barabara ya Morogoro na Samnujoma
S.L.P. 9524,
DAR-ES-SALAAM

Tafadhali bonyeza linki ifuatayo ili uweze kuona majina ya walioitwa kwenye usaili:

KUITWA_KWENYE_USAILI_-_EDITED_-_HRM_2014-10-06.pdf


0 comments:

Post a Comment