Shirika lisilo la kiserikali la Help for Underserved Communities Inc. (HUC), limetangaza nafasi za ufadhili wa masomo ya ufundi VETA kwa vijana wa Kitanzania.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo, leo, inasema, HUC, itafadhili wanafunzi 15 za kozi za awali VETA kwa mwaka 2014-2015.
Walengwa ni vijana waliomaliza shule za msingi ambao wamethibitika kuwa wazazi/walezi wao wameshindwa kuwalipia ada. Imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, mwanafunzi atatakiwa kujaza kwa usahihi fomu ya maombi (chini), akiambatanisha na barua akieleza sababu za kuomba ufadhili huu na barua ya utambulisho toka ofisi ya serikali za mitaa na mwisho wa kupokea barua za maombi ni Jumatano, Oktoba 01, 2014, saa 11 jioni.
Barua za maombi zitumwe kupitia:
Maombi ya ufadhili wa masomo,
Help for Underserved Communities Inc.
P. O. Box 7022,
Dar es Salaam,
Tanzania.
Au
Help for Underserved Communities Inc.
P.O.Box 6822,
Ellicott City, MD 21042
Au
Kupitia baruapepe:
info@myhuc.org OR kijasti@hotmail.com
Taarifa hiyo imesema, majina ya watakaopata ufadhili yatatangazwa Oktoba 10, 2014 na kwamba ada italipwa moja kwa moja chuoni.
HUC ni shirika lisilo la kiserikali toka nchini Marekani lenye lengo la kuziwezesha jamii zipatazo huduma hafifu kupata maji safi na salama, vifaa vya elimu na ufadhili wa masomo ya ufundi. Mwaka jana, shirika hili lilifadhili vijana 11 VETA.

0 comments:
Post a Comment