Sunday, August 24, 2014

Tangazo kwa wote waliochaguliwa kujiunga JKT - Septemba 2014



Tangazo kwa wote waliochaguliwa kujiunga JKT - Septemba 2014
Tangazo lililotolewa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, JKT, linasema kuwa, jeshi la Kujenga Taifa linawatangazia vijana wote waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa Sheria kuwa wanatakiwa kuripoti kwenye makambi waliyopangiwa kuanzia tarehe 04 Septemba 2014 kwa mafunzo yatakayoanza rasmi tarehe 11 Septemba 2014.

Aidha, tangazo hilo linasema kuwa JKT inakanusha uvumi unaosambazwa kwa kutumia ujumbe mfupi wa njia ya simu "SMS" na kwenye mitandao ya kijamii kuwa mafunz hayo hayatakuwepo. Taarifa hii si ya kweli bali ni uzushi na upotoshaji.

Inasisitizwa kuwa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria ni lazima. Atakayeshindwa kuripoti atakuwa
amevunja sheria na atachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na JKT kwenye tovuti yake, wanaotakiwa kuripoti ni kama ifuatavyo:-

  1. Walimu wote wa ngazi ya cheti (GATCE) 2014 (waliohitimu mwaka 2014)
  2. Wallimu elfu tatu wa ngazi ya Diploma (DSEE) (waliohitimu mwaka 2014)
  3. Vijana wa Kidato cha Sita ambao hawajaandika barua za kuomba kuahirisha kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa hapo awali.

Majina ya vijana na vikosi valivyopangiwa yanapatikana katika tovuti ya JKT: www.jkt.go.tz


TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA.


Related Posts:

  • Next Generation Leaders Programme Manager Job Title : Next Generation Leaders Programme Manager Source : Restless Development Requirements : � Relevant graduate or post-graduate degree (Degree, Masters, or Diploma) � Strong knowledge of current and future devel… Read More
  • Finance and Administration ManagerJob Title : Finance and Administration Manager Source : Restless Development Requirements : Essential � Excellent excel skills for production and analysis of complex budgets and expenditure reporting � Be numerate and detail… Read More
  • Youth Policy and Advocacy Coordinator TanzaniaJob Title : Youth Policy and Advocacy Coordinator Tanzania Source : Requirements : � Graduate or post-graduate level degree (Degree, Masters, or Diploma) � Excellent IT skills � in MS Word, Excel, PowerPoint (and preferabl… Read More
  • Human Resources Officer - Performance Statistics_TANESCOJob Title : Human Resources Officer - Performance Statistics Source : The Guardian, October 4, 2011 Requirements : Bachelor's degree in Business Administration/Statistics or related Degree from recognized higher learning… Read More
  • Southern Highlands Programme ManagerJob Title : Southern Highlands Programme Manager Source : Restless Development Requirements : � Graduate or post-graduate level degree (Degree, Masters, or Diploma). � Strong knowledge of current and future development tren… Read More

0 comments:

Post a Comment