Monday, August 25, 2014

AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RORYA - 8/25/2014


AJIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA RORYA - 8/25/2014
Kutoka Gazeti la Mwananchi 25 August
Kwa Mujibu wa Kibali cha Ajira Na CB 170/377/01/E/52 cha tarehe 16 Julai, 2014 kutoka kwa Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya RORYA anawatqngazia wananchi wote wenye sifa ambao ni raia wa Tanzania kuomba nafasi za kazi kama ifuatavyo:-

Mlinzi - Nafasi (01) (a) 
Sifa:
(i) Awe na uwezo wa kusoma na kuandika.
(ii) Awe amehitimu Kidato cha nne na kufaulu mafunzo ya Mgambo/Polisi/JKT au mafunzo ya
Zimamoto kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali. (iii) £,we raia wa Tanzania.
(b) Kazi na Majukumu:
(i) Atawajibika kwa mwangalizi wa Ofisi.
(ii) Atahakikisha kuwa hakuna mali ya ofisi inayotoka nje ya ofisi bila idhini au kibali. (iii) AtahaRikisha kuwa mali yoyote inayoingizwa ofisini inazo hali za uhai wake.
(iv) Atalinda usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku.
(v) Kuhakikisha kuwa wageni wote wanaoingia katika eneo la ofisi wana idhini ya kufanya hivyo. (vi) Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea katika sehemu za kazi kama vile moto,mafuriko
n,k na kutoa taarifa katika sehemu zinazohusika.
(vii) Kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha ulinzi mahali pa kazi. (c) Mshahara: TGOS A yaani shilingi 265'000 na Kuendelea.

Msaidizi Wa Ofisi (Office Assistants) NAFASI MOJA - (01) (a) 
Sifa:
(i) Awe raia wa Tanzania.
(ii) Awe wahitimuwa wa kidato cha nne (IV) waliofaulu vizuri katika masomo ya kiingereza, Kiswahili na Hisabati.
(iii) Wawe waadilifu, wabunifu na wawajibikaji. (b). Kazi na Majukumu.
(i) Kufanya usafi wa ofisi na Mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja na kufagia, kufuata vumbi, kupiga deki, kukata majani, kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanga maua na miti na kusafisha vyoo.
(ii).Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwa maofisa wanaohusika na kuyarudisha
sehemu zinazohusika.
(iii) Kusambaza barua za ofisi kama jinsi watakavyo elekezwa. (iv) Kutayarisha chai ya ofisi.
(iv) Kupeleka mifuko ya posta na kuchukua barua kutoka posta.
(v) Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinawekwa sehemu zinazostahili,kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati wa Asubuhi na Jioni kuyafunga baada ya Saa za Kazi.
(vi) Kudurufu barua au rnachapisho kwenye mashine za kudurufia na kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.
(e) Mshahara: TGOS A (yaani 265,000 na kuendelea.

 Mtendaji Kijiji (III) NAFASI TANO (5)
(a) Sifa.
(i) Awe Raia wa Tanzania.
(ii) Awe na elimu ya Kidato cha IV na VI na amehitimu mafunzo ya Astashahada(Cheti) kwa miaka miwili katika fani yoyote kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali .
(b) Kazi na Majukumu.
(i) Atakuwa . Mtendaji na mshauri mkuu wa serikali ya Kijiji na kamati zake katika mipango ya maendeleo ya kijamii na utekelezaji wa mipango ya Maendeleo.
(ii) Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia mapato na Matumizi ya Serikali ya
Kijiji.
(iii) Atakuwa Mlinzi wa Amani na msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
(iv) Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji Mipango ya Maendeleo ya Kijiji. (v) Atakuwa Katibu wa Halmashau Kijiji.
(c) Mshahra: TGS B yaani 345,000 na Kuendelea.

APPLICATION INSTRUCTIONS:

MAMBO VA JUMLA YA KUZINGATlA.
1. Waombaji wawe na umri kati ya miaka 25-40.
2. Waombaji wote waambatanishe vivuli vya vyeti vyao kwenye barua za maombi, pia waandike
Namba zao za Simu.
3. Barua zibandikwe picha mbili za (Stamp size)
4. Usaili, wataarifiwa tarehe wale watakaotimiza masharti yaliyotajwa.
5. Maombi vote yatumwe kwa anuani ifuatayo.

Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya
S.L.P 250,
TARIME/Rorya.
6. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15/09/2014 saa 9.30 alasiri na maombi yatakayowasilishwa baada ya muda huo hayatapokelewa.
Gerald N Ruzika
Katibu Bodi ya Ajira
Rorya


0 comments:

Post a Comment