Wednesday, July 2, 2014

Nafasi za Kazi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ,Julai 2014



Nafasi za Kazi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ,Julai 2014
Kumb. Na EA.7/96/01/G/27 1 Julai, 2014

Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 100 kwa ajili ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

1.0 MKAGUZI WA HESABU DARAJA LA II (AUDITOR GRADE II) - NAFASI 100 

1.1 MAJUKUMU YA KAZI

Kukagua nyaraka za matumizi, maendeleo, amana, wakala, mfuko, miradi maalum na mapato ya Serikali.

Kushiriki kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mpango wa kazi za ukaguzi wa kila mwaka.


NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i.      Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45

ii.       Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii.       Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv.      Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

v.      Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)

watatu wa kuaminika.

vi.    Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya

kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.

-      Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

-      Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

-      Computer Certificate

-      Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

-      Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vii.      Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)

HAVITAKUBALIWA.

viii.      Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

ix.      Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

x.      Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi.      Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xii.       Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 15 Julai, 2014

xiii.       Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv.      Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.




Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika

Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,

Secretariat,
SLP.63100,

P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

Dar es Salaam.


0 comments:

Post a Comment