Wednesday, July 2, 2014

MKUFUNZI MIFUGO DARAJA II (ANIMAL SCIENCE) – NAFASI 3



MKUFUNZI MIFUGO DARAJA II (ANIMAL SCIENCE) – NAFASI 3
Mkufunzi Mifugo Daraja Ii (Animal Science) – Nafasi 3

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kutafsiri mihutasari ya mafunzo kwenye masomo.
• Kuandaa mtiririko wa kila somo (Lesson Plan) kwa upande wa nadharia na vitendo.

7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Sayansi ya Mifugo kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
7.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.

Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 877 za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
-Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates. -Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI -Computer Certificate -Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) -Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 11 Julai, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
 


APPLICATION INSTRUCTIONS:

Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma
S. L. P 63100,
DAR ES SALAAM.


0 comments:

Post a Comment