Monday, June 23, 2014

Wasimamizi wa huduma za wagonjwa nyumbani (HBC Focal person)



Wasimamizi wa huduma za wagonjwa nyumbani (HBC Focal person)
TANGAZO LA KAZI
COMMUNITY CONCERN OF ORPHANS AND DEVELOPMENT ASSOCIATION-(COCODA)
17/6/2014

Shirika la COCODA linapenda kuwatangazia nafasi za kazi kwa wale wote wenye taaluma ya uuguzi ambao wako tayari kufanya kazi na shirika letu.
JINA LA MRADI: TUNAJALI II

JINA LA KAZI: Wasimamizi wa huduma za wagonjwa nyumbani (HBC Focal person)
WANARIPOTI: Kwa Mratibu Mradi
NAFASI: Tatu (3)
SIFA ZA MWOMBAJI
Ø  Awe amehitimu mafuzo ya uuguzi katika ngazi ya stashahada(diploma) au Astashahada (cheti )kozi ya miaka miwili au zaidi katika chuo kinachotambulika na serikali.
Ø  Awe raia wa Tanzania
Ø  Umri usiozidi miaka 40
Ø  Awe na uwezo wa kuongea na kuandika Kingereza na Kiswahili
Ø  Awe na ujuzi wa komputa
Ø  Maombi yote yaambatanishwe :Nakala ya cheti cha taaluma/nakala ya cheti cha kidato cha nne /sita maelezo binafsi (CV) picha ( passport size  mbili) za hivi karibuni pamoja na cheti cha kuzaliwa
Ø  Mwombaji awe tayari kufanya kazi Wilaya yoyote atakayopangiwa ndani ya mkoa wa Njombe.
Ø  Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 26 Juni, 2014


MAJUKUMU YA KAZI

1. Kumsaidia mratibu mradi kutekeleza shughuli za huduma za wagonjwa nyumbani.
2. Kusimamia na kuelekeza  kwa vitendo  kwa wahudumu wa kujitolea wakati wote wa utekelezaji wa shughuli zilizopo kwenye mpango kazi wa huduma za wagonjwa nyumbani.
3. Kuwezesha upatikanaji wa wagonjwa waliopotea CTC na PMTCT kwa kushirikiana na watu wa vituo vya afya na wasimamizi wa huduma za wagonjwa nyumbani.
4. Kuwezesha na kugawanya vitendea kazi na misaada ya kijamii kwa wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi kusimamia utunzaji mzuri na matumizi yake.
5. Kuwawezesha na kuwapa rufaa wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi kwenda kwenye vituo husika na misaada mingine  kwa ajiri ya huduma na msaada Zaidi
6. Kushirikiana na  mratibu mradi pamoja na wafanyakazi wengine,kutengeneza mtandao na kushirikiana na taasisi nyingine pamoja na mashirika mengine ndani ya wilaya zinazoingiliana na kuwezesha shughuli za huduma za wagonjwa nyumbani
7. Kuandika vitu unavyojifunza wakati wa kutekeleza shughuli za  huduma za wagonjwa nyumbani ndani ya mradi wa TUNAJALI kwa kushirikiana na mratibu kwa ajiri ya kutolea taarifa TUNAJALI mkoa /TUNAJALI makao makuu
8.Kuwasaidia wahudumu wa wagonjwa nyumbani kufuatia mafunzo na  ufuatiliaji kwa yale waliyojifunza.
9.Kuimalisha vikundi vipya vya WAVIU na kuweka na kukopeshana kuwawezesha kujisajiri na kuwaunganisha na taasisi nyingine kwa misaada Zaidi.
10.Kusimamia ukusanyaji wa takwimu na taarifa kutoka kwa wahudumu wa kujitolea na kutoa mrejesho katika uchambuzi wa takwimu
11.Kuandaa taarifa za utendaji za mwezi, robo mwaka, na za mwaka.
12.Kufanya shughuli zozote utakazopangiwa zinazohusiana na mahitaji ya mradi wa TUNAJALI

Barua inaweza kuandikwa  lugha ya Kiswahili au Kingereza,barua zote zitumwe kwa njia ya posta kupitia anuani ifuatayo;-

How to Apply

Meneja shirika la COCODA
S.L.P 712
NJOMBE


0 comments:

Post a Comment