Saturday, May 24, 2014

ziara ya Profesa Mwandosya nchini Burundi



ziara ya Profesa Mwandosya nchini Burundi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum)  Profesa Mark Mwandosya,wa pili kulia, amekuwa na mazungumzo na Waziri wa Mawasiliano ya Simu,Habari,na Uhusiano na Bunge,wa Burundi,Mhe.Tharcisse Nkezabahizi,watatu kulia, na Francois Sigejeje,Katibu Mkuu wa Wizara yake,wa nne kulia.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Prof. Mark k Mwandosya ,wa tano kushoto ametembelea Mamlaka ya Maji na Umeme ya Burundi(REGIDESO) mjini Bujumbura.Pamoja naye ni Liberat Mfumukiko,wa sita kushoto.Wengine ni ujumbe wa Waziri na maafisa wa REGIDESO.
Prof.  Mwandosya amekuwa na Mazungumzo na Waziri wa Elimu ya Msingi na Sekondari wa Burundi Mheshimiwa Dr Rose Gahiru,aliye katikati.Kulia ni Bw.Samuel,Mshauri wake.

Waziri Mwandosya,wa tatu kulia,amekutana na viongozi wa Chama cha Wasafirishaji wa Kimataifa wa Burundi(ATIB) kuhusu changamoto zinazowakabili nchini Tanzania.Wengine kuanzia kulia ni Bw.Eric Ntagazo,Mtendaji Mkuu, Melchior Niyonzima,Mwenyekiti,Nd.Elias Tamba,Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Burundi,Natasha Ndimana,Katibu Mkuu,na Ainue Rwankineza,Makamu wa Mwenyekiti.
Ofisini kwake,Waziri wa Mawasiliano ya Simu,Habari na Uhusiano na Bunge wa Burundi Mhe.Tharcisse Nkezabahizi,kushoto,amemwonesha  Waziri Mwandosya orodha ya waliowahi kuwa Mawaziri wa Wizara hiyo kuanzia mwaka 1962 mpaka 2012.
Baada ya kutembelea Wizara ya Elimu ya Msing na Sekondari Bujumbura,Waziri Mwandosya na Waziri Dr Rose Gahiru na Nd.Elias Tamba,Kaimu Balozi wa Tanzania walio katikati wakiwa na na maafisa wa Serikali za Tanzania na Burundi


0 comments:

Post a Comment