Kiongozi wa UNDP, na Waziri Mkuu wa zamani wa New Zealand, Helen Clark(pichani), amewapongeza viongozi wa vyama vya siasa Tanzania kwa dhamira yao ya kuwasimamisha wanawake zaidi, vijana na watu wenye ulemavu kama wagombea kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwaka 2015. Alitoa pongezi hizo wakati wa mkutano wake na Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda, na wabunge wanawake katika mji mkuu wa kisiasa wa Dodoma leo.
Kiongozi huyo wa UNDP amekutana na wabunge wanawake wa Tanzania huko Dodoma, akiwemo Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda, katika jengo la Bunge, mjini Dodoma.
Helen Clark aliwapongeza wabunge wanawake kutokana na huduma yao bungeni na taifa wakati akielezea mshikamano na msaada kwa ajili ya maendeleo ya wanawake katika utawala wa kidemokrasia, siasa na maisha ya umma, na kubadilishana uzoefu katika majadiliano na kuelezea malengo na dhamira ya UNDP kwa maendeleo ya wanawake, ikiwa ni pamoja na siasa.
'Tanzania ipo mstari wa mbele katika ahadi ya kuboresha ushiriki katika siasa kwa makundi yaliyotengwa kutokana na dhamira ya vyama vya siasa kufanya hivyo katika uteuzi wa wagombea kwa uchaguzi wa mwaka ujao,' alisema. 'UNDP ina furaha kutoa msaada kwa hili kwa kushirikiana na Wanawake wa Umoja wa Mataifa na kundi la mashirika ya kitaifa.'
Helen Clark alitoa shukrani hizo wakati wa mkutano na Kundi la Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Shirika lisilo la Kiserikali la wanawake wote Wabunge, kutoka vyama vyote vya siasa. Aliwapongeza wabunge wanawake kuhusu huduma zao kwa Bunge na taifa wakati akielezea mshikamano na msaada kwa ajili ya maendeleo ya wanawake katika utawala wa kidemokrasia, siasa na maisha ya umma.
Kundi la Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) ni jukwaa la wabunge wa vyama vyote na kusajiliwa kama shirika lisilo la kiserikali na linafanya kazi ndani na nje ya bunge. Linajumuisha wanachama wote wa kike wa bunge bila kujali muelekeo wao wa kisiasa. Kundi hili hupokea fedha kutoka kwa wafadhili na hujenga uwezo wa wabunge wanawake, kuwawezesha kutoa utendaji bora katika bunge na kuwa na uaminifu mkubwa kama wanasiasa. Hii ni kutofautiana na mtazamo wa jadi wa Tanzania kwamba "wanawake ni watu wa jikoni.'
'Hii imekuwa fursa ya kipekee na maalumu ya kubadilishana uzoefu na kuelezea malengo na dhamira ya UNDP ya maendeleo ya wanawake, ikiwa ni pamoja na katika siasa,' alisema. Clark ni mbunge wa zamani, Waziri, kiongozi wa chama na Waziri Mkuu kwa mihula mitatu.
UNDP inasaidia maendeleo ya uwezo wa Bunge na Baraza la Wawakilishi Zanzibar kupitia mradi unaofadhiliwa na wafadhili. Shughuli za mradi huu zinalenga Wajumbe wa mabunge yote mawili, Kamati za Bunge, na Sekretarieti. Mradi huu unasimama juu ya mafanikio ya mabunge yenyewe na msaada uliotolewa awali na UNDP na washirika wa wahisani.
0 comments:
Post a Comment