Jana Jumanne, Wake za Mabalozi na Wake za Maafisa wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa, waliandaa United Nations International Bazaar, Bazaar hiyo iliyohusisha bidhaa za aina mbalimbali vikiwamo vyakula ilifanyika katika viunga vya Umoja wa Mataifa hapa New York. Mapato yatakayotokana na mauzo ya bidhaa na vyakula pamoja na tiketi za bahatinasibu yatakepelekwa katika Mfuko wa Maafa pamoja na Kusaidia Mradi Maalum wa Watoto. Baadhi ya Wake wa Maafisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa wakiongozwa na Mke wa Balozi, Bibi. Upendo Manongi walishiriki Bazaar hiyo. Zifuatazo ni baadhi ya Taswira za tukio hilo
Sehemu ya Umati uliofika kwenye bazaar hiyo na kununua au kuangalia bidhaa mbalimbali
Baadhi ya Wake wa Maafisa wa Uwakilishi wa Kudumu wakiongozwa na Mke wa Balozi, Bibi Upendo Manongi (mwenye miwani) wakiwa katika picha ya pamoja. Banda la Tanzania lilikuwa na vyakula vya asili ya kitanzania, kama vile maandazi na vitumbua, vitafunwa vilivyochangamkiwa sana na waliofika kushuhudia Bazaar hiyo.
Mdau akinunua maandazi.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi naye hakucheza mbali, hapa akiwa na akina Mama wakati alipofika katika Banda lao.
Mke wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bibi Yoo Soon-Taek, akivishwa skafu ya bendera ya Tanzania wakati alipokuwa akitembelea mabanda mbalimbali na kufika banda la Tanzania.
washiriki wengine nao wakiwa wamepanga bidhaa zao.
Sehemu ya Washiriki wengi waliojitokeza kutoka Wakilishi Mbalimbali za Kudumu.
0 comments:
Post a Comment