Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Manju Msambya akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sambaru kwenye hafla hiyo ya makabidhiano ya leseni tatu.
Na Hillary Shoo,
KAMPUNI ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Shanta Mining Ltd, imetoa leseni tatu na mtaji wa shilingi milioni 40 kwa kikundi cha wachimbaji wadogo cha Aminika cha kijiji cha Mang'onyi Wilayani Ikungi Mkoani Singida.
Kikundi hicho Aminika Gold Mine Co- Operative Society Ltd Mang'onyi kimekabidhiwa leseni hizo jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stepheni Maselle kwenye kijiji cha Sambaru.
Akikabidhi leseni hizo Naibu Waziri Maselle liwataka wanakikundi kujipanga vizuri katikakuanza kufanya kazi ya uchimbaji dhahabu ili kujikwamua kimaendeleo.
Aidha alisema ni matarajio yake kuona kuwa kikundi hicho kinakuwa na maendeleo na kuwa mfano wa kuigwa hapa nchini, kwani tayari nguvu kazi wamepewa mtaji na Shanta.
Naibu Waziri wa Nishati na madini Steven Maselle akizungumza na wananchi wa kijiji cha Samabru Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida wakati wa makabidhiano ya leseni tatu kwa wanakikundi cha Aminika Ltd.
"Ndugu zangu sijui mungu awape nini, mmepewa leseni, mmepewa mtaji na vifaa vya kuanzia kazi na hawa wenzetu wa Tan Discovery, mnaoneshwa eneo ambalo tayari limefanyiwa utafiti, sasa kazi kwenu." Alisema Maselle huku akishangiliwa na wananchi.
Aidha aliwataka wanakikundi hao kutumia kama SACCOS katika kukopa sehemu mbalimbali za kifedha kwa manufaa yetu na kizazi cha baadae.
Hata hivyo Naibu Waziri, Maselle alisema ni dhamira ya serikali kuendeleza wachimbaji wadogo hapa nchini, kwa kuwapatia mafunzo na namna bora ya uchimbaji madini.
Katika risala ya wanakikundi cha Aminika iliyosomwa na Katibu wake Hamis Kingi alisema kikundi hicho ni muungano wa vikundi vitano kutoka vijiji vitatu vitakavyoathirika na Mgodi wa Kampuni ya Shanta Mining vyenye jumla ya wanachama 218.
Katibu wa kikundi cha Aminika Ltd akimkabidhi zawadi ya Mbuzi jike Naibu Waziri wa Nishati na madini Steven Maselle.
Kingi alivitaja vikundi hivyo kuwa ni Elimika Sambaru,Amani Sambaru, Amka Sambaru, Aminifu Mang'onyi na Muungano Mlumbi ambavyo kwa pamoja vimeungana na kuwa kikundi kimoja kinachojulikana kwa jina la Aminika
Aidha alitanabaisha kwamba vikundi baada ya maelekezo hayo ya Serikali wachimbaji waliendelea kujiunga pamoja na kuunda kikundi kilichofuata utaratibu wa kisheria wa kusajiliwa na kupata usajili namba, SIR624 Kikundi cha Aminika Gold Mine Co – Operative Society Ltd – Mang'onyi hatimaye wamekabidhiwa rasmi na Serikali.
"Mh,Naibu Waziri wa Nishati na Madini kwa kuwa kikundi kiko Kisheria tunaomba Serikali kupitia Wizara yako ya Nishati na Madini Makubaliano yetu kati ya Kampuni na Kikundi cha Aminika yaweze kutekelezeka kwa muda mwafaka, kwani wanakikundi wanahitaji kufanya kazi ili kujikwamua kiuchumi."Alifafanua Kingi.
"Pia tunakushukuru wewe binafsi kwa juhudi zako kubwa kuwatetea wachimbaji wadogo kwa kupitia Wizara ya Nishati na Madini." Alisema.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Steven Maselle akimkabidhi Mmoja ya wanakikundi Aminika Ltd cha kijiji cha Mang'onyi Wilayani Ikungi Sprian Danford ,moja ya leseni tatu za uchimbaji wa madini ya dhahabu zilizotolewa na Kampuni ya Shanta Mining Ltd, katika hafla fupi za makabidhiano iliyofanyika Kijiji cha Sambaru.
Kikundi cha ngoma ya Kinyaturu cha Muungano Ikungi wakitumbuiza kwenye sherehe za makabidhiano ya leseni.
Hapa mkuu wa kampuni ya kukopesha vifaa ya Tan Discovery Tanzania Roges Sezinga akitafsiri kwa lugha ya kishwahili kwa wananchi hotuba ya CEO wa Shanta.
Huyu Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya Shanta Mining Ltd Tanzania, Mike Houston.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Hassan Tati akiagana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Maselle.( PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO).
0 comments:
Post a Comment