Wednesday, May 21, 2014

Rais Dkt Shein Atembelea Bandari ya Malindi Unguja.

 
 
 
 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Abdalla Juma (katikati) alipofanya ziara ya kutembelea katika Ofisi ya Shirika hilo leo Wilaya ya Mjini Unguja,(kushoto) Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Seif Rashid,(kulia) Naibu Waziri Issa Haji Gavu, na (wapili kulia) Katibu Mkuu Wizara hiyo Juma Akili
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Maliasili Affani Othman Maalim (kulia) alipotembelea Ghala linalomilikiwa na Wizara hiyo akiwa katika ziara ya kutembelea Maghala mbali mbali katika bandari ya Unguja leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Maafisa wa Shirika la Biashara ZSTC alipotembelea maghala yanayomilikiwa na Shirika hilo katika  Bandari ya malindi Unguja leo alipofanya ziara maalum.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu Wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Julian Raphael (kulia) alipokuwa akiangalia mashine ya kushindika karafuu ambayo kwa hivi sasa ikiwa katika hali ya uchakavu na kutofanya kazi,wakati alipofanya ziara ya kutembelea maghala ya karafuu yaliyopo Bandarini malindi Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa  Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Abdalla Juma (katikati) alipofanya ziara ya kutembelea eneo la kuhifadhia Makontena katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
 
 

0 comments:

Post a Comment