Thursday, May 29, 2014

MMLIKI WA MANCHESTER UNITED AFARIKI DUNIA …mashabiki nusu huzuni, nusu furaha …hajawahi kukubalika Old Trafford



MMLIKI WA MANCHESTER UNITED AFARIKI DUNIA …mashabiki nusu huzuni, nusu furaha …hajawahi kukubalika Old Trafford

Owner: Malcolm Glazer has died at the age of 85

MALCOLM Glazer, aliyeinunua Manchester United kwa utata mwaka 2005, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85.

Mfanyabiasha huyo wa Kimarekani atakumbukwa kwa muda mrefu kama milionea aliyeichukua Manchester United miaka tisa iliyopita katika ununuzi uliouingiza klabu katika deni la mkopo wa zaidi ya pauni milioni 500.

Ingawa Glazer alikuwa mgonjwa na kuiacha klabu iendeshwe na watoto wake Joel na Avram, alikuwa ndiyo mtu aliyeongoza manunuzi ya Manchester United kinyume na matakwa ya mashabiki wa timu.

Unpopular: Manchester United fans hang anti-Glazer                  banners in 2010

Moja ya mabango ya mashabiki wa Manchester United yaliyokuwa yanampinga Glazer

Kutakuwa na majonzi lakini kunategemewa kuwa na huruma ndogo tu kutoka kwa mashabiki wengi wa United ambao siku zote wamekuwa wakimshutumu Glazer kwa kuiingiza klabu kwenye madeni makubwa.

Glazer ameacha mke na watoto sita.



0 comments:

Post a Comment