Tuesday, May 13, 2014

MDAU AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZA IPTL NA WAZIRI WA MADINI NA NISHATI SOMA HAPA MWENYEWE FACTS LIVE!!

 
 
 
 
TUHUMA zinazotolewa hivisasa kwenye vyombo mbalimbali vya habari nchini na kuihusisha wizara ya Nishati na Madini, imebainika nyuma yake kuna nguvu ya wafanyabiashara na wanasiasa wanaopigania maslahi yao binafsi kwenye mashirika yaliyo chini ya Wizara hiyo.
 
Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili limezipata, wabunge na wafanyabiashara hao hivisasa wameungana ili kufanikisha mipango yao ya kuipaka matope wizara ya Nishati na Madini na serikali ya awamu ya nne iliyo chini ya Rais Jakaya Kikwete.
 
Mmoja wa wafanyabiashara ambaye ametajwa kwenye vita hiyo ni Reginald Mengi, ambaye mbali na kumiliki vyombo vya habari amekuwa akijihusisha na masuala ya uchimbaji wa madini ambapo kwa sasa anamiliki vitalu vya utafutaji madini 54 vyenye ukubwa kwa KM2 2,958.65 sawa na ukubwa wa Mkoa wa Dar es Salaam mbili.
 
Aidha, Mengi anamiliki leseni mbili za uchimbaji vito za Kampuni mbili ambazo ni Tanzanite Africa Limited zote zipo Wilaya ya Simanjiro, Mkoa wa Arusha.
 
Pamoja na kumili Kampuni hizo za uchimbaji Madini Mkoani Arusha na Mikoa Mingine lakini mfanyabiashara huyu halipi kodi wala Mrabaha kama ambavyo wachimbaji wengine hufanya akidai kwamba hajawahi kupata kitu wakati wa uchimbaji wake wa madini.
 
Wakati akiendelea kuhodhi vitalu vingi vya madini ambavyo havifanyii kazi wala kuchimba madini bado anahangaika kwa kupita huku na ule kushawishi makundi mbalimbali ya watu wamsaidie kupata vitalu vya gesi ambavyo akatafute wawekezaji yeye ili baadaye aweze kujipatia fedha yeye na familia yake.
 
Kutokana na kugonga mwamba katika kipindi hiki kupitia kwa Waziri wa Nishati ambaye amegoma watu binafsi wachache wamiliki vitalu ambavyo watakuwa madalali kwa kuleta wawekezaji ili wafaidike wao binafsi badala ya kufaidika Watanzania wote ndiyo sababu inayomsukuma Mengi pamoja na wengine kuanza kuipaka matope Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Waziri wake.
 
Inadaiwa Mengi na wafanyabiashara wenzake wamekuwa wakipigania kupata vitalu zaidi vya uchimbaji wa gesi ambavyo serikali imekuwa ikisema, uchimbaji na utafiti wake unagharimu fedha nyingi ambazo wafanyabiashara wa ndani hawana uwezo wa kufanya shughuli hiyo.
 
Taarifa zaidi zinasema, wakati mengi akipigania vitalu hivyo kwa madai ya kutaka kuwanufaisha wazawa, inadaiwa lengo la mfanyabiashara huyo na wenzake ni kuchukua vitalu hivyo na kufanya ulanguzi wa mafuta na gesi.
 
Mfanyabiashara huyo mbali na kuwa kiongozi wa sekta binafsi nchini, pia ana maslahi ya moja kwa moja na biashara ya utafutaji, uchimbaji na uvunaji wa rasilimali za madini, mafuta na gesi.
 
 
"Kama kuna mtu anaamini mengi na wenzake wanapigania vitalu ili kuwanufaisha wazawa kama anavyodai, atakuwa anakosea, Mengi na wenzake wanataka kuchukua vitalu ili wafanye ulanguzi wa gesi na mafuta yetu, hawana uzalendo kiasi hicho kwa watanzania" kilisema chanzo chetu kutoka serikalini (jina tunalihifadhi).
 
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa, kinachomfanya Mengi hivisasa atoe tuhuma kwa serikali hususani kwa waziri Muhongo ni kile anachoamini, waziri huyo anakwamisha mipango yake ya kutaka kumiliki vitalu zaidi na kumkosesha mamilioni ya fedha.
 
Taarifa zaidi zinadai, katika kufanikisha vita yake hiyo, Mengi ameungana na mwanasheria maarufu nchini Nimrod Mkono ambaye hivi sasa kampuni yake ya Mkono and Company Advocates imenyimwa kazi ya kuitetea TANESCO iliyoshitakiwa na kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
 
Imeelezwa tayari mkono kupitia kampuni yake hiyo imechota zaidi ya bilioni 52 tangu mwaka 2008 hadi 2013, lakini ilinyimwa kazi hiyo baada ya kubainika kushirikiana na washitaki kulihujumu TANESCO katika kesi hiyo.
 
Kutokana na uamuzi huo, Mkono inadaiwa amepania kuipaka matope serikali kwa kushirikiana na watu wenye mgogoro na Wizara ya Nishati na Madini akiwemo Mengi na mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto Kabwe ambaye naye inadaiwa amekuwa na ugomvi na Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Eliakim Maswi.
 
Inadaiwa Maswi aliingia kwenye mgogoro na Zitto wakati wa sakata la tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zilizomkabili aliyekuwa mkurugenzi wa TANESCO William Muhando.
 
Aidha, Zitto ndiye anadaiwa kumtumia Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila katika kuishambulia serikali na wizara ya nishati na madini, ambapo hivikaribuni amewatuhumu mawaziri wawili kuchota Sh200 bilioni katika Akaunti ya Escrow, iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Tanesco na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL.
 
"Hakuna asiyejua kwamba Kafulila anatumiwa na Zitto, tangu yupo Chadema hadi ametoka amekuwa akimtumia, sasa anamtumia hadi kwenye masuala yake binafsi ikiwemo kwenye vita yake na Maswi" kilisema chanzo chetu kutoka Chadema.
 
Taarifa zaidi zinadai, siku chache zilizopita, Zitto na Kafulila walikuwa na kikao cha siri nyumbani kwa Nimrod Mkono ambapo kikao hicho kinadaiwa ni kupanga mikakati ya kukabiliana na serikali baada ya Mkono kukosa tenda ya kuitetea TANESCO na Zitto kulipiza kisasi kwa ugomvi wake na Maswi.
 
"Kinachoonekana hasa kwenye hizi tuhuma zinazotolewa hivisasa zaidi ni maslahi ya watu, mkono ana hasira na serikali hasa na wizara ya nishati kwa kukosa tenda, mengi naye anapigania kupata vitalu, Zitto yeye analipiza visasi kwa Maswi"
 
"Kwa hali hii sijui kama tutafika, ukiwaona watu wakisimama bunge na kwenye majukwaa mbalimbali wakitoa kauli kali na kutoa tuhuma unaweza kudhani ni wazalendo, kumbe wana mambo yao binafsi" alisema mtumishi mmoja wa serikali ambaye jina lake hakupenda litoke gazetini.
 
Mtumishi huyo alisema, imekuwa kawaida hivisasa watu wakikosa maslahi kwenye mashirika ya umma, kukodi watu na vyombo vya habari kushambulia wengine na wakati mwingine wamekuwa wakishambulia hata wenyewe malengi mazuri na taifa.
 
"Bado sijaona tatizo la Prof. Muhongo, kinachofanyika hapa ni fitna, kuna watu wamezoea kufanya wanachotaka na kuliibia taifa, sasa wamedhibitiwa wanaanza vita ambazo hazina msingi, nakumbuka Rais Kikwete aliwahi kusema hakuna mzawa atakayezuiwa kuwekeza, sijui hofu ya mengi na wenzake na kufikia hatua ya kuwapaka matope hata wasio na hatia"

0 comments:

Post a Comment