Tuesday, May 13, 2014

LUKE SHAW KUTUA MANCHESTER UNITED KWA PAUNI MIL 27 …ategemewa kumpora namba Evra

 
 
 
 
 

All over: Shaw said his goodbyes to the Saints fans after the 1-1 draw with United at St Mary's

MANCHESTER United itamsani beki wa kushoto wa Southapmton Luke Shaw kwa dau la pauni milioni 27.

Wakati akitajwa kwenye kikosi cha England kitakachokwenda Kombe la Dunia, Shaw alikuwa mbioni kukamilisha usajili wake wa kwenda Old Trafford. Dili hilo linategemewa kutangazwa mapemba kabla mashindano ya Kombe la dunia hajaanza nchini Brazil.

Licha ya kumaliza katika nafasi ya saba kwenye Ligi Kuu msimu huu, United iko na matumani ya kushinda mbio za kumnasa beki huyo mwenye umri wa miaka 18 anayewaniwa pia na Manchester City na Chelsea.

Shaw anategemea kuwa beki tatu chaguo la kwanza Old Traffrod akimrithi Patrice Evra, jambo linaloongeza ushawishi wa yeye kutua United licha ya kuwa kocha mpya bado hajatangazwa.

United haitaki kurudia makosa ya msimu uliopita iliposhindwa kufanya usajili wa maana.

0 comments:

Post a Comment