Monday, September 9, 2013

MAKOSA 10 WANAUME HUYAFANYA WAKIWA FARAGHA -2


MAKOSA 10 WANAUME HUYAFANYA WAKIWA FARAGHA -2
 
LEO naendelea na mada ya makosa kumi ambayo wanaume wamekuwa wakiyafanya faragha. Tuwe pamoja...
Mwanaume hana budi kumsoma mwanamke wake.

 
Ajue nini afanye, wapi na wakati gani ili ampatie. Tatizo wengi wanakariri kutokana na mazoea au stori za hadithi njoo uongo njoo utamu kolea. Elewa kuwa 'kutuama' kifuani kwa muda mrefu siyo suluhisho.
Inawezekana ukawa fundi wa kucheza dakika nyingi lakini ukawa unashindwa kumpa starehe, kinyume chake ukawa kero. Badala ya kumfanya apende tukio la ninyi kukutana, akalichukia kabisa. Dawa namba moja ni kubadili mtazamo wako kuhusu mapenzi.
Kwa bahati mbaya, wanaume wengi huishia kutokuwa na taarifa sahihi kuhusu namna bora ya kuwafurahisha wanawake faragha. Kwa nafasi yangu kama mshauri, nikiwa nimekutana na watu wengi, nimeweza kugundua kwamba wanawake wengi wanaweza kuvumilia tatizo la kutofikishwa kileleni kwa muda mrefu bila kuzungumza popote.
Sasa basi, kwa vile ipo wazi kwamba wanawake hushindwa kujieleza hata kama hawaridhiki na kitendo, ni jukumu la mwanaume kuvunja ukimya na kuujua ukweli hasa. Tatizo mojawapo la wanaume ni kushindwa kutafuta majibu ya jambo hili.
Tuwe wakweli kwamba kuna wapenzi wengi katika maeneo mbalimbali, wanaongozwa na kanuni ambazo hudhani ndiyo inafaa kuzitumia kwa mtu yeyote. Mwanaume unatakiwa uwe umemjua mwanamke wako kisha uwe na kanuni ambazo utazitumia kwake tu.
Wanaume kwa wingi wao, hushindwa kutambua ukweli kwamba wanawake nao huwa na hitaji la kitendo cha faragha. Kutokana na kasoro hiyo, huwa hawaelewi kipindi gani mwanamke anakuwa hataki kabisa kusikia kitu mapenzi.
Pale mwanamke anapokuwa anahitaji hasa kitendo, utakuta mwanaume anakuwa 'bize' bila sababu za msingi. Hata wanapokutana hufanya kwa masilahi yake binafsi pasipo kuzingatia  nafsi ya mwenzake. Matokeo yake, mwanamke anashtuka mchezo umekwisha wakati yeye hajaonja raha hata kiduchu.
Silaha namba moja ni kuheshimu hisia zake. Tambua kwamba naye ni binadamu, kwa hiyo analo hitaji la juu kabisa la kitendo cha faragha na ni jukumu lako kumkata kiu. Ukiishi kwa mazoea ni tatizo, ndiyo maana wengi wanasaidiwa na wanaume wengine jinsi ya kuwahudumia wanawake wao faragha.
Yapo makosa mengi lakini nimeyaweka pamoja katika vipengele 10. Naamini ndani yake, nimegusa maeneo yote muhimu ambayo hasahasa ndiyo yanayowaangusha wanaume. Nikuombe tu kwa unyenyekevu, ufuatilie kwa makini.

KUFIKIRI WANAFURAHIA KITENDO WAKATI SIYO KWELI
Wanawake wana utani sana, anaweza kuangusha mayowe na kujitikisa kuonesha namna anavyosisimka kumbe hamna lolote. Anaweza kulia kwa sauti ya juu kwamba anafika kileleni wakati siyo kweli. Hufanya hivyo ili kukufurahisha wewe mwanaume.
Wanajua kwamba wanaume hujiona wapo ngangari pale wanapowafikisha wanawake wao kileleni. Sasa basi, ikitokea mchezo anaona ni mrefu na hafurahii chochote, huamua kuifanya mechi ifike tamati kwa kudanganya amefika kileleni kisha anamtaka na mwanaume wake naye amalize.
Soma mawazo haya ya mwanamke huyu ambaye ni msomaji wangu: "Kuna maeneo ambayo mwanaume wangu akiyagusa ndipo nafika kileleni. Katika wanaume niliowahi kukutana nao, wote wana staili moja. Hawanipatii.
Itaendelea wiki ijayo.



0 comments:

Post a Comment