Tuesday, September 3, 2013

FAO LA URITHI NSSF LAWAVUTIA WANAFUNZI MAONESHO YA VODACOM ELIMU EXPO 2013


FAO LA URITHI NSSF LAWAVUTIA WANAFUNZI MAONESHO YA VODACOM ELIMU EXPO 2013
WANAFUNZI waliojitokeza katika Maonesho ya Vodacom Elimu Expo 2013 wamefurahishwa na huduma zinazotolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), hususani katika Fao la Urithi.

Fao hilo lililowafurahisha mno wanafunzi hao, linawawezesha watoto wenye umri chini ya miaka 18 hadi 21 kunufaika, huku likiwawezesha kupata asilimia 60 ya mgao wa mwanzo endapo mtegemezi anapofariki.


Akizungumzia sababu zinazowafanya wanafunzi kuifurahia huduma ya Fao la Urithi, Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga alisema kuwa fao hilo limekuwa mkombozi kwa wanafunzi kwa kuwawezesha katika elimu pindi mtegemezi anapofariki, hivyo kuwanufaisha watoto walio mashuleni. 

"Mwanachama endepo akifariki asilimia 60 ya mgao wa mwanzo unakwenda kwa watoto wasiozidi 4 wenye umri chini ya miaka 18 hadi 21 ambao wapo mashuleni  kwa ajili ya kujiendeleza kielimu, hii imewafanya wengi miongoni mwa wanafunzi kuvutiwa na huduma hiyo," alisema Kapinga.

 NSSF imeanzisha matibabu ya bure kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu ambapo imeingia mkataba na hospitali za vyuo kupitia Fao la SHIB, ambalo linamuwezesha mwanafunzi wa chuo kupata huduma za matibabu bure, endapo mwanafunzi atachangia sh. 20,000 kwa mwezi. 

NSSF pia hutoa mikopo ya Elimu kupitia Saccos ambapo wanachama wanaweza kukopa kuanzia milioni 50 hadi bilioni 1.
Wanafunzi wakipata maeleo mbalimbali kuhusiana na Fao la Urithi, ambalo linamuwezesha mtoto chini ya umri wa miaka 18 hadi 21 kupata asilimia 60 ya mgao wa mwanzo wa ambapo ,wanachama atafariki kwa ajili ya kumuwezesha katika elimu.
 Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dk.  Didas Masaburi, kuhusu Fao la Urithi ambalo linamuwezesha mwanafunzi kupata asilimia 60 ya mgao wa mwanzo endapo mtegemezi atafariki kwa ajili ya kumuwezesha katika masomo yake,  wakati wa Maonesho ya Vodacom Elimu Expo 2013 yaliyofanyika kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni Ofisa Matekelezo NSSF, Rose Kayombo. 
Kutoka kulia ni Ofisa Matekelezo NSSF, Rose John Kayombo, Ofisa Idara ya Kompyuta, Grace Magigita na Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga.



0 comments:

Post a Comment