Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Thea alisema miaka kadhaa iliyopita alitabiri kuwa wasanii waliokuwa wanavuma sana ambao walitokea kwenye mashindano ya u-miss, hawatadumu kwenye uigizaji hivyo utabiri wake umetimia kwani sasa hivi, hawavumi tena.
"Utabiri wangu unafanya kazi kwa sababu kwa sasa wale wasanii walioibukia kwenye mashindano ya u-miss wengi hawasikiki tena, wasanii wanatakiwa kutambua kuwa sanaa hii siyo lelemama yaani mpaka kufikia hapa tulipo tulifanya kazi ya ziada, tulisota sana kwenye vikundi," alisema Thea.
0 comments:
Post a Comment