MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Aman Temba 'Mheshimiwa Temba' aweka wazi kuwa baadhi ya wasanii wanaotumia dawa za kulevya wanakosa akili na matokeo yake kuwa machizi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Temba aliweka wazi kuwa baadhi ya wasanii wanaotumia dawa hizo akili zao zinakuwa haziko sawa na kuonekana wa ajabu hata kwa jamii inayowazunguka.
Alisema wanaotumia hizo dawa utawagundua kutokana na matendo yao wanayoyafanya kuonekana kama wamerukwa na akili hata kama wanajificha.
"Mimi ningekuwa natumia dawa za kulevya ungenigundua tu kwani hata usingeweza kuongea na mimi wala kunifanyia mahojiano yoyote kwa njia ya simu, kwani wengi wao wanaotumia dawa hizo wanakosa ustaarabu kabisa" alisema Temba.
Aliongezea kuwa hawezi kutumia dawa hizo kwani bado anahitaji heshima na kujua malengo yake, hivyo hata hao wanaoacha kutumia dawa hizo ni bora wakatambua ni sababu zipi zilizowapelekea kujiingiza katika matumiz hayo.
CHANZO CHA HABARI HII NI MDAU PRO24
0 comments:
Post a Comment