Rais wa Kenya, Mhe., Uhuru Kenyatta amewazima wanasiasa wanaotaka kumwita Mtukufu Rais, akisema enzi za sifa hizo zilipita.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Gatundu, Rais Kenyatta alisema wanaotaka kumpatia sifa, wanaweza kumwita Mheshimiwa Rais na wala sio Mtukufu Rais, ambalo Mstaafu, Mtukufu Rais Daniel Moi hakujali kuitwa hivyo na wanasiasa katika shughuli za kiserikali
Rais Kenyatta nusura amkatize Seneta wa Kiambu, Bw Kimani Wamatangi, aliyerudia mara kadha kumtambua kama Mtukufu Rais: "Ninajua washirika wangu wa kisiasa hapa wanapenda serikali yao, lakini ninataka kumwambia Seneta Wamatangi kwamba siku hizi hatutambui jina mtukufu. Ukitaka sema Mheshimiwa Rais," akasema Rais Kenyatta huku akishangiliwa.
Alionekana kufuata hatua ya Rais mstaafu Mwai Kibaki, aliyekataa hadharani kuitwa mtukufu.
Awali, Rais Kenyatta alisema Kenya itaendelea kushirikiana na Uchina katika maendeleo. Read More

0 comments:
Post a Comment