FAMILIA ya Mzee Augustino Mgonja wa Pugu Kajiungeni Dar es Salaam na Familia ya Marehemu Bwana na Bibi Henry Kitosi (Mwakitosi) wa Iringa zinasikitika kutangaza kifo cha Mtoto wao, VICTORIA KITOSI (DOTTO) kilichotokea Alfajiri ya leo Agosti 22, 2013 katika Hopitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam alikolazwa baada ya kuugua ghafla.
Mipango ya Mazishi inafanyika Pugu Kajiungeni nyumbani kwa Mjomba wake Agustino Mgonja.
Habari ziwafikie, Mama Mdogo wa Marehemu, Mary Nathan wa Kinyenze Kipera Mkoani Morogoro, Kaka wa Marehemu Bosco Kitosi wa Mwanza,Doris KitosiA wa Iringa, Bibi wa Marehemu,Balozi Christina Shogholo wa Kisiwani Same-Kilimanjaro, Mjomba John Mgonja wa Kabuku Tanga, Ukoo wote wa Mwakitosi na Shogholo, Ndugu Jamaa na Marafiki popote pale walipo.
Marehemu ameacha Mume na watoto wawili, Sanden na Sabri.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. AMEN.
0 comments:
Post a Comment