Shiria la habari la Reuters linasema Snowden alikwamba kuondoka kiwanja cha ndege cha Urusi kuelekea Havana, Cuba kutokana na shinikizo la Marekani.
Gazeti moja ya nchini Urusi limesema Snowden ambaye anatakiwa nchini Marekani ili kujibu tuhuma za kutoa habari za siri za nchi hiyo kuhusu programu yake ya kufuatilia mawasiliano ya watu mbalimbali, alishindwa kwenda Havana siku ya pili baada ya kutua Moscow kama ilivyokuwa imepangwa baada ya maafisa nchini Cuba kuwaambia maafisa wa kiwanja cha ndege cha Urusi dakika ya mwisho kabisa, kumzuia Snowden asipakie ndege ya Aerolflot kuelekea kwao, pamoja na kuwa tayari alikuwa abiria mwenye siti.
Gazeti hilo (Kommersant) limeendelea kubainisha kuwa Snowden pia aliishi siku kadhaa kwenye ubalozi wa Urusi uliopo nchini Hong Kong ambapo maafisa wake waliripoti kuwa uamuzi wa kwenda kwenye ubalozi wao ulikuwa wa kushitukiza na hawakuwa na taarifa wala mipango yoyote. Akiwa humo, Snowden pia alibainisha wazi kwa maafisa hao kuwa nia yake ni kwenda katika mojawapo ya nchi za Amerika ya Kusini kupitia Moscow na hivyo anaomba msaada na ulinzi wao.
Snowden anaishi nchini Urusi kama mkimbizi kwa visa ya mwaka mmoja kuanzia mwezi jana.
Habari kamili ipo Reuters.com

0 comments:
Post a Comment