Sunday, August 25, 2013

Nissan yazuia basi lililokatika breki kutokuleta maafa




Nissan yazuia basi lililokatika breki kutokuleta maafa
Basi moja la kampuni ya Mrisho Investment juzi lilifeli breki zake na kuanza kuserereka hadi lilipopunguzwa mwendo na kusimama baada ya kuvaa ubavu wa gari dogo aina ya Nissan.

Tukio hilo linasimuliwa kuwa lilitokea huko Temeke Sudani jijini Dar es Salaam juzi.

Hakuna aliyeripotiwa kujeruhiwa ama kuumia kulikoweza kuonekana kwa macho.

---
wavuti.com inashauri kuwa, baada ya ajali, ni vyema mtu akaenda hospitalini kwa ajili ya vipimo vya uchunguzi zaidi wa viungo vya ndani ili kujithibitishia na kuridhika kuwa hakuna viuongo vyovyote vya ndani ya mwili vilivyoshituka ili kuepusha madhara ya kiafya yanayoweza kujitokeza baadaye au hata kifo cha ghafla kwa kutokupata tiba haraka. Ni rahisi sana kwa mtu aliyepona ajalini kujikagua na kujiona hana neno wala hajisikii maumivu kwa kuwa haoni jeraha lolote, lakini kwa bahati mbaya akawa ameumiza vidonda vya ndani ambavyo huharibika taratibu na kushindwa kufanya kazi yake.
Picture
Gari aina ya Nissa likiwa limesukumwa hadi nje ya barabara baada ya basi la Mrisho Investment kufeli breki na kuligonga.
Picture
Mwenye Nissan (T-shirt Nyeusi) akielezea jinsi gari lake lilivyosukumwa na basi kutoka barabarani (picha via JF)



0 comments:

Post a Comment