Wednesday, August 14, 2013

Ngoma Africa band yatiisha International African Tubingen 2013, Ujerumani



Ngoma Africa band yatiisha International African Tubingen 2013, Ujerumani
Mzimu wa Dansi "Ngoma Africa Band umetimiza miaka 20 na bado unatisha!

Mabalozi wa kiafrika nchini Ujerumani wamewapongeza FFU wa Ngoma Africa Band kwa kuchukua tena International Diaspora Award 2013 Bendi bora ya Kiafrika Ulaya.

Ngoma Africa Band ilifanikiwa kuutetea ubingwa wake wa bendi bora na kujichukulia Tuzo ya kimataifa ya IDA mjini Tubingen, Ujerumani katika maonyesho ya kimataifa ya International African Festival Tubingen 2013.

Bendi hiyo maarufu kwa kuwatia kiwewe washabiki na mdunduko wake imevunja rekodi kwa kuwa na washabiki wa kimataifa kila pembe.

Usikose kuwasikiliza FFU kupitia www.ngoma-africa.com, picha zaidi zimepachikwa hapo chini...



0 comments:

Post a Comment