MUIGIZAJI aliyejipatia umaarufu katika tamthilia ya 'Prison Break' Wentworth Miller maarufu kwa jina la 'Michael Scolfield' ameamua kujitangaza rasmi kuwa yeye ni shoga.
Muigizaji huyo ameamua kuweka wazi kitendo hicho baada ya kupokea barua ya mwaliko wa kuhudhuria tamasha la filamu la kimataifa lililotarajiwa kufanyika St. Petersburg nchini Urusi
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kupitia mtandao wa 'People.com' imeweka wazi kuwa Scolfield amekataa mwaliko huyo wa kuitembelea nchi hiyo kutokana na sheria zao zinazowabana wanaume wanaojihusisha na ushoga.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa baada ya muigizaji huyo kuipokea barua hiyo ya mwaliko ndipo alipoamua kuijibu kwa kuweka wazi kuwa kitendo cha nchi hiyo kuweka sheria ya kuwabana mashoga ndio sababu kubwa inayompelekea kushindwa kuhudhuria tamasha hilo.
"Nashukuru kwa mwaliko wenu, mimi nina asili kiasi ya Urusi ingenipa faraja sana kuitembelea nchi hiyo, lakini kutokana na sheria zenu mimi nikiwa kama shoga lazima niukatae mualiko huo" aliandika Scolfield na kuongezea kuwa."Ninaumiwa kwa kiasi kikubwa na jinsi mashoga wanavyotendewa na serikali hiyo".
Scolfield alieleza kuwa kutokana na sheria hiyo na jinsi serikali ya nchi hiyo inavyowachukulia mashoga hao hawezi kushiriki kwa amani kwenye tukio hilo lililoandaliwa na nchi inayowanyanyasa watu kama wao ikiwa pamoja na kuwanyima haki yao ya msingi ya kusihi.
Mwezi June nchi hiyo ilianzisha sheria dhidi ya ushoga iliyosainiwa na rais wa nchi hiyo Vladimir Putin ambayo imezua mijadala ya wazi jinsi sheria hiyo inavyokataza wapenzi wa jinsia moja.
Wentworth ni muigizaji aliyejipatia umaarufu kwenye tamthilia ya Prison Break mnamo mwaka 2005 hadi 2009, ingawa ameweza kushiriki pamoja na kuandaa filamu nyingine tofauti tofauti ikiwemo 'Stoker'.
0 comments:
Post a Comment