TAKRIBAN kombamwiko milioni moja wametoroka kutoka kwenye shamba walimokuwa wakifugwa nchini China ili kuweza kutumika kwa dawa za kienyeji, ripoti imesema.
Mende hao walitoroka kutoka kwa shamba hilo eneo la Dafeng, mashariki mwa mkoa wa Jiangsu mapema mwezi huu, na kuelekea kwenye mashamba ya mahindi yaliyopo karibu, baada ya mtu asiyejulikana kuharibu sehemu ambapo walikuwa wanafugwa, gazeti la Modern Express lilisema.
Wakuu wa kudhibiti maradhi wametuma wapelelezi watano katika eneo hilo kutoa mpango wa kuwaondoa.
Mmiliki wa shamba hilo Wang Pengsheng aliwekeza zaidi ya KSh1.3 milioni katika kilo 102 za mayai ya Periplaneta americana baada ya kuunda mpango wa biashara wa miezi sita, ripoti ilisema.
Mende kwa kawaida huchukuliwa kama mdudu lakini wanaoamini dawa za kienyeji za Wachina hutumia mimea na pia wanyama ambao ni pamoja na viumbe vilivyopo hatarini wakisema kuwa vinaweza kutibu kansa, kupunguza uvimbe na kumarisha kinga dhidi ya maradhi.
Kufikia wakati ambapo kinyumba cha plastiki ambapo walikuwa wakifugiwa kiliharibiwa, kulikuwa na kombamwiko zaidi ya milioni 1.5 waliokuwa wameanguliwa na walikuwa wakilishwa chakula ambacho ni pamoja na "matunda na biskuti" kila siku, Wang alinukuliwa akisema.
Bw Wang alisema kuwa alikuwa ametarajia kutengeza zaidi ya KSh14,000 kama faida kwa kila kilo ya kombamwiko ambayo angeuza, lakini sasa anakabiliwa na hasara kubwa. --- Swahilihub.com

0 comments:
Post a Comment