Wednesday, August 14, 2013

CHADEMA yaendelea na Mabaraza ya Katiba Mpya katika maeneo tofauti



CHADEMA yaendelea na Mabaraza ya Katiba Mpya katika maeneo tofauti
Mabaraza ya Katiba Mpya ya CHADEMA ambayo yanafanyika kwa uwazi kwenye mikutano ya hadhara, ambapo wananchi wote wanapata fursa ya kushiriki kujadili Rasimu ya Katiba Mpya, kutoa maoni yao na kutia saini kwenye fomu zilizoandaliwa kwa ajili ya kazi hiyo, yanaendelea leo katika maeneo tofauti tofauti.

Zikitumia usafiri wa anga (chopper) timu mbili, zikiongozwa na viongozi wakuu, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Slaa zitafanya mikutano katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Simiyu na Kilimanjaro, baada ya jana kufanyika katika mikoa ya Mara na Kilimanjaro.

Timu hizo ambazo zote zina wataalam wa masuala ya katiba, leo zitakuwa na ratiba ifuatayo:-
Timu ya Mwenyekiti; Busega (saa 3 asbh), Maswa (saa 5 asbh), Meatu (saa 7 mchana) na itamalizia Bariadi (saa 10 jioni)

Timu ya Katibu Mkuu; Moshi Vijijini/Kibosho (saa 4 asbh) Hai/Bomang'ombe (saa 6 mchn), Siha/Sanya Juu (saa 8 mchn) na itamalizia Moshi Mjini saa 10 jioni.

Wananchi wote wanaombwa kujitokeza kujadili mstakabali wa maisha yao kwa miaka 50/100 ijayo namna gani wanataka kujitawala na kuongozwa, kwa kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba Mpya.

Wakati huo huo maelfu ya wananchi wameitikia wito wa kuendelea kutoa maoni yao kupitia simu ya mkononi kwa kutuma ujumbe mfupi kwenye namba 0789 24 82 24 na kwenye email hii: chademamaoni@gmail.com

Kwa jana mwitikio ulikuwa ni mkubwa sana kama inavyoonekana katika picha.



0 comments:

Post a Comment