Thursday, August 29, 2013

Askofu Moses Kulola




Askofu Moses Kulola
Taarifa zilizochapishwa kwenye blogu ya GospelKitaa zinasema:

Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika ambazo Gospel Kitaa imezipata kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.

Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dk Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.

Gospel Kitaa itaendelea kukufahamisha kwa kadri ambavyo taarifa zitakuwa zikitufikia.

Ili kufahamu historia ya maisha ya Hayati Askofu Dr. Moses Kulola, tafadhali bofya hapa.

BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.



0 comments:

Post a Comment