Saturday, October 13, 2012

Mtangazaji mkongwe wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani Othman Miraji astaafu baada ya utumishi wa miaka 35


Baada ya miaka 35 ya utumishi wa uaminifu katika Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani, Othmani Miraji ijumaa hii, 12.10.2012, ilikuwa siku yake ya mwisho kazini kama mhariri mwandamizi.Wafanyakazi wenzake, wakiongozwa na mhariri mkuu wa DW, Bibi Ute Shaeffer, na pia mkuu wa matangazo ya Kiswahili, Bibi Andrea Schmidt, walimfanyia karamu murua ya kumuaga na kumtakia kila la heri na afya njema katika maisha yake ya baadae. Pia walisifu mchango mkubwa alioutoa katika kuifanya DW iwe kuinganisho cha kupata habari za kuaminika na mototo kutoka duniani kote na katika kuikuza lugha ya Kiswahili. Othman Miraji alijiunga na DW akitokea idara ya kunasa matangazo ya BBC Monitaring service, Nairobi, Kenya, mwaka 1977 ambako alitumika kwa miaka saba.
Mtangazaji mkongwe wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani Othman Miraji (kulia) akizungumza na Mhariri Mkuu wa Idara ya Afrika ya Deutsche Welle, Ute Schaeffer (kushoto) na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Andrea Schmidt. Othman Miraji ameagwa rasmi leo kufuatia kustaafu baada ya kuitumikia Idhaa hii kwa miaka 35. Picha zote na mdau Sudi Mnete
Mtangazaji mkongwe wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani Othman Miraji akipokea zawadi toka kwa Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Andrea Schmidt. 
Bango ofisini DW
Mstaafu akiwa na wadau wakuu wa DW
wadau wa DW wakipiga mduara wakati wa hafla hiyo


Related Posts:

0 comments:

Post a Comment