Tuesday, September 25, 2012

MKUU WA MKOA WA MWANZA AFUNGUA RASMI MAONYESHO YA 33 YA UTALII DUNIANI KITAIFA JIJINI MWANZA


Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akifurahia nembo inayowakilisha mkoa huo katika suala zima la maonyesho ya shughuli za utalii kwenye ufunguzi wa maonyesho ya 33 ya siku ya Utalii duniani ambapo kitaifa mwaka huu 2012 yanafanyika Mwanza.

Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akisalimiana na moja kati ya waratibu wa maonyesho ya Siku ya Utalii Bi. Ester ambapo kitaifa yanafanyika jijini Mwanza ambapo leo ilikuwa siku ya ufunguzi.

Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akigusa ngoma kama ishara ya ufunguzi wa jadi kwa maonyesho ya kitalii jijini Mwanza, mtindo huu ni tofauti na ule wa ukataji utepe.

Mpiga mbiu aina ya Bigra aliipiga kama ishara ya sauti ya kualika watu kuhudhulia tambiko moja kati ya mila za watu kabila la wasukuma.

Wanyama Mtemi Ilago, alitambika pande zote nne kuita neema kwa shughuli za utalii mkoa wa Mwanza, inatajwa kuwa mtemi huyu ndiye kwa siku ya leo asubuhi alitumika kuita mvua na kisha akaistopisha ilishuguli za Maadhimisho ya Utalii ziendelee.

Meza kuu ikifurahia jambo.
Kushoto ni mkuu wa wilaya mpya ya Busega Paulo Mzindakaya akiwa na wakuu wengine kwenye jukwaa la wageni maalum katika Maadhimisho ya 33 ya Utalii yaliyofunguliwa rasmi leo na mkuu wa mkoa huo Evarist Ndikilo katika viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza .

''''''Ngoma inogileeee'''' Ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) hakuona hasara kujitosa kuicheza ngoma ya wakali kutoka jumba la makumbusho ya kabila la watu wa Sukuma Bujora.

Mwonekano muhimu.....

Kwa karibu wanasomeka Mariam Lugaila (mkuu wa wilaya ya Misungwi), na Jacline Liana mkuu wa wilaya ya Magu wakiwa  Jukwaa kuu Uwanja wa Nyamagana katika Maonyesho ya 33 ya Utalii duniani kwa mara ya kwanza Kitaifa yakifanyika jijini Mwanza.

Utalii na ngoma zetu asili.

Kundi hili linaitwa 'Ngoma ya Mang'ombe ya kijiji'

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo kwenye hotuba yake ameiomba Kamati ya Tume ya Taifa ya Utalii kuipa nafasi tena Mwanza kwa mwaka ujao iwe mwenyeji wa maonyesho kama hayo ili kukomaza vyema katika shughuli za utalii sambamba na kupata fursa ya mwendelezo wa kutangaza vivutio vya utalii na shughuli zake zilizopo mkoani humo.

Wadau wa masuala ya utalii wakimsikiliza kwa dhati mkuu wa mkoa.

Burudani jukwaani ni Rock City Band ambao waliimba wimbo maalum wa vivutio vya utalii mkoa wa Mwanza..

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali kujionea shughuli ziambatanazo na utalii hapa alikuwa banda la Utalii Malaika Hotel Mwanza akitambulishwa huduma nyingine za kunogesha utalii zilizoongezwa.

0 comments:

Post a Comment