Tuesday, August 14, 2012

WATATU WAFUKUZWA KUTOKANA NA KASHFA YA KUUZA WANYAMA NJE YA BONGO.


.

Waziri wa Maliasili na utalii amewafukuza kazi watumishi wake watatu wanaotuhumiwa kuhusika na kashfa ya kusafirisha wanyama hai kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwenda nje ya nchi.

Waziri wa maliasili Balozi Khamis Kagasheki amesema ingawa anakumbana na upinzani mkali kutoka kwa wana mtandao, atahakikisha anasimamia haki katika kusafisha uozo ndani ya wizara hiyo.

Waliofukuzwa ni Mbagwa Mkurugenzi wa wanyama pori, Ofisa wa uwindaji wa kitalii Arusha Simon Ngwera na watatu ni Frank Mremi ambae pia ni Ofisa uwindaji wa kitali.

Kwenye line nyingine balozi Kagasheki alikanusha na kutolea ufafanuzi kuhusu ishu za baadhi ya wabunge kumuhusisha na ufisadi ambao umefanywa na miongoni mwa watendaji kabla ya yeye kuteuliwa kuwa waziri wa wizara hiyo.

Source:TBC


0 comments:

Post a Comment