Kwanza poleni sana katika kipindi hiki kigumu cha kuchukuliwa mkali Robin van Persie ambae ameingia kwenye familia ya Alex Ferguson.
Ninachotaka kuwaambia ni ripoti ya gazeti la The Sun Uingereza kuandika kwamba kocha Arsene Wenger wa Arsenal amesisitiza kwamba hatonunua striker mwingine ili kuchukua nafasi ya Robin Van Persie.
Yani kasema washambuliaji Olivier Giroud na Lukas Podolski wanatosha kabisa kuziba nafasi ya Van Persie na muda wote wawili hao walikua wakiandaliwa kuchukua hiyo nafasi.
Kocha huyo Mfaransa mwenye miaka 62 toka aletwe duniani, amesema japo inauma kupoteza mchezaji kama Van Persie kulikua hakuna njia yoyote isipokua kumuuza tu.
Kwenye line nyingine ni kwamba kocha wa Manchester United amesema anaamini jumatatu Van Persie atacheza kwenye mechi dhidi ya Everton.
August 15 2012 usiku ndio ilithibitisha kumchukua Van Persie ambapo Fergie alithibitisha kwamba mkali huyo alitarajiwa kufika Old Traford August 16 jioni kuonana na madaktari wa club hiyo na ana imani yote yaliyobakia yatamalizika kabla ya mechi ya jumatatu.
Kwa kumalizia amefananisha uwepo wa Wyne Rooney, Van Persie, Chicharito na Danny Welbeck kama ilivyokua 1999 kwa uwepo wa vichwa vikali kama Yorke, Cole, Sheringham and Solskjaer — the four best strikers in Europe.
0 comments:
Post a Comment