Wafanyakazi wa Karakana ya Wonder wakinyanyua moja ya nembo (logo) iliyotengezwa kwa vyuma chakavu
Meneja Usalama wa mahali pa kazi Renatus Nyanda (kushoto) akisaidia kufunga mlango wa Pick Up baada ya kupakia vyuma chakavu vilivyokusanywa kiwandani hapo kwa ajili ya kutengenezea vifaa
Fundi Mchundo (Welder), Seif Chambela akiwa na sanamu ya tembo iliyotengenzwa kwa kutumia vyuma chakavu katika Karakana ya Wonder (Wonder Workshop)Wafanyakazi wa Karakana ya Wonder (WonderWorkshop), Msasani, Dar es Salaam Meneja Mradi wa Wonder Workshop, Lisette Westerhuis, akimuonesha Meneja Mawasiliano na Habari wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi, sanamu ya ndege aliyetengenezwa kwa kutumia vyuma chakavu hivi karibuni katika karakana hiyo iliyopo Msasani, Dar es Salaam. TBL itakuwa inaipatia kila mara Karakana hiyo vyuma chakavu na makasha kwa ajili yakutengenezea vifaa mbalimbali zikiwemo sanamu za wanyama.
Meneja Mawasiliano na Habari wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (kushoto) akiwasaidia wafanyakazi wa Karakana ya Wonder,Nico Ngalawa (kulia) na Hafidh Selemani wakipakia kwenye gari vyuma chakavu walivyopewa msaada na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), vilivyokusanywa juzi katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Ilala Mchikichini, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment