Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro Tanzania , Carlos Msigwa akipongezwa na Diwani wa kata ya Mkundi Emelda Chambo, baada ya kumkabidhi msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni 4,8 kwa ajiri ya shule ya msingi ya Ujirani iliyopo kijiji cha Kienge B, Manispaa ya Morogoro.
Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos Msigwa akiteta jambo na Kulwa Mussa (12) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Ujirani iliyopo kijiji cha Kienge B Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni4.8 na Benki ya KCB Tanzania,Katikati ni Meneja Masoko wa benki hiyo Imelda Gerald.
Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos Msigwa wa pili kutoka (kulia) akipongezwa na Mkuu wa shule ya msingi ya Ujirani Philemon Kibuja, iliyopo kijiji cha Kienge B katika Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni4.8. na benki ya KCB Tanzania,wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Mshauri wa shule Godfrey Tairo na Mwalimu wa kujitolea Lazaro Isondo.
Meneja wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, Carlos akiteta jambo na wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi Ujirani iliyopo kijiji cha Kienge B katika Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhiwa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni4.8.
Afisa Masoko wa Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro,Herieth Mwakifulefule akimsaidia kumvisha kiatu Kulwa Mussa, ambaye ni Mwanafunzi wa darasa la Tatu katika shule ya msingi ya Ujirani ya jamii ya wamasai iliyopo katika kijiji cha Kienge B, baada ya benki hiyo kutoa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni4.8. mtoto huyo tangu darasa la kwanza amekuwa akishika nafasi ya kwanza katika darasa lao.
Wanafunzi wa jamii ya kimasai wa Shule ya msingi ya Ujirani iliyopo kijiji cha Kienge B katika Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro, wakiwa na furaha baada ya Benki ya KCB Tanzania kuwakabidhi msaada wa madawati80 yenyethamani ya shilingi milioni 4.8.Shule hiyo inajumla ya wanafunzi 400.kwa mara yakwanza ndio wameanza kukalia madawati.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya KCB Tanzania imetoa msaada wa madawati 80 yenye thamani ya shilingi milioni nne na laki nane (4.8m) kwa shule ya msingi Ujirani iliyopo katika kata ya Mkundi manispaa ya Morogoro.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati hayo, Meneja wa KCB Tawi la Morogoro Carlos Msigwa alisema kuwa lengo la msaada huo lilikuwa kusaidia upungufu wa madawati katika shule hiyo na hivyo kuwawezesha wanafunzi kusoma vizuri
Meneja huo alisema kuwa Benki ya KCB inatambua umuhimu wa elimu bora katika maendeleo ya taifa na ndiyo maana haikusita kuelekeza msaada huo katika sekta ya elimu.
Akipokea msaada huo, diwani wa kata ya Mkundi Emelda Chambo aliishukuru Banki ya KCB kwa kutoa msaada na kusema kuwa utakuwa chachu kubwa katika maendeleo ya elimu katika shule hiyo ambayo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa madawati.
Tuaishukuru sana KCB kwani wamekuwa kama walezi kwa shule yetu. Hii ni mara ya tatu kupokea msaada baada ya ule wa miti ya kivuli pamoja na vitabu.Tunaahidi kuyatunza madawati haya ili mtakaporudi tena myakute katika hali nzuri.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Philemon Kibuja shule hiyo yenye wanafunzi 400 imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ukosefu mkubwa wa madawati.
"Mimi ndiyo mwalimu mkuu na mwalimu pekee katika shule hii. Nafundisha kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Shule hii kabla ya kupata msaada huu kutoka KCB haikuwa na dawati hata moja. Wanafunzi walilazimika kukaa chini, kwenye magogo na kwenye mabenchi,' alisema
Mwalimu huyo aliishukuru Benki ya KCB na kuomba serikali pamoja na makampuni binafsi kuidia shule hiyo ambayo wanafunzi wengi wanatoka katika jamii za wafugaji.
"Shule hii yenye wanafunzi 400 ina madarasa matatu tu na mwalimu ni mimi peke yangu. Pamoja na jitihada kubwa ya kuomba msaada serikalini, serikali haijaweza kutusaidia. Tunaomba mashirika mbalimbali kujitikeza kutusaidia," alisema
0 comments:
Post a Comment