HATIMAYE lile bifu kati ya mwandishi mkongwe wa mkoani Iringa, Francis Godwin na msanii Diamond Platinum, limekwisha baina yao baada ya kufikia muafaka wa kufuta kesi ya madai aliyofunguliwa msanii huyo. Wakiongea katika kikao cha usuluhishi kilichofanyika ndani ya ofisi za Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho, Godwin ameamua kumsamehe Diamond na kuahidi kufuta kesi. Diamond amemuomba msamaha Godwin kwa yote yaliyotokea ambapo imebainika kwenye kikao hicho kuwa aliyesababisha uhasama kati yao alikuwa ni mtu mwingine waliyemtegemea kumaliza mgogoro wao, lakini badala yake aliwasaliti na kujenga chuki miongoni mwao, lakini kuanzia sasa ieleweke kuwa bifu lao limekwisha.
PICHANI ni Diamond (mwenye T-shirt nyekundu) na Godwin (mwenye suti) wakipeana mikono mara baada ya kikao hicho, huku wakishuhudiwa na Mrisho (kushoto) na mzee Mbizo (kulia) mara baada ya kufikia muafaka ofisini kwa Meneja Mkuu.
PICHA: Issa Mnally/GPL
0 comments:
Post a Comment