Saturday, May 12, 2012

AIRTEL YATOA MSAADA WA MADAWATI NA MIPIRA KWA SHULE ZA MSINGI JIJINI DAR


Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza Quinton Fortune, akikabidhi moja ya mipira iliyotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maarifa Mareitha Mulyalya huku Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Mh Kassim Majaliwa akitazama. Kampuni ya Airtel Tanzania ilitoa mipira 30, jezi seti tatu na madawati 40 kwa shule za msingi za Maarifa, JICA na Mwangaza zote za Gongo La Mboto, Dar es Salaam.

Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza Quinton Fortune, akikabidhi moja ya madawati yaliyotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Maarifa Mareitha Mulyalya huku Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Mh Kassim Majaliwa akitazama. Kampuni ya Airtel Tanzania ilitoa mipira 30, jesi seti tatu na madawati 40 kwa shule za msingi za Maarifa, JICA na Mwangaza zote za Gongo La Mboto, Dar es Salaam.

Msanii wa kizazi kipya Ambwene Yesaya maarufu kama AY, akiwatumbuiza wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Maarifa iliyopo Gongo La Mboto nje kidogo Jijini Dar es Salaam wakati Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ilipotoa msaada wa madawati 30, mipira ya miguu 40 na jezi seti tatu, Alhamisi Mei 10, 2012 ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mtaa (Elimu) Mh. Kassim Majaliwa. Shule zingine zilizofaindika na msaada ni Maarifa, JICA na Mwangaza zote za Gongo La Mboto, Dar es Salaam.

Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza Quinton Fortune, akifurahia na wanafunzi wa shule ya Msingi ya Maarifa baada ya kukabidhi madawati 30, mipira 40 na jesi seti tatu zilizotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania. Shule zingine zilizofaidika na msaada huo ni pamoja na Mwangaza na JICA zote za Gongo La Mboto, jijini Dar es Salaam. Msaada huo ulikabidhiwa na Naibu Waziri wa Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa Kassim Majaliwa, Alhamisi Mei 10, 2012.


0 comments:

Post a Comment