Sunday, April 8, 2012

MDOGO WA KANUMBA AFUNGUKA,LULU AGOMA OYSTERBAY POLICE STATION

MDOGO WA KANUMBA AFUNGUKA,LULU AGOMA OYSTERBAY POLICE STATION

Ndugu wa Marehemu Steven Kanumba,Seth,ameelezea mkasa uliopelekea kifo cha kaka yake kilichotokea usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Sinza Vatican.Akielezea mbele ya waandishi wa habari Seth alisema kwamba Lulu alifika nyumbani kwa Kanumba usiku huo na baadae wakaanza kuzozana na Steven.Baada ya muda mfupi wote Kanumba na Lulu wakaingia chumbani. Baada ya dakika chache Lulu alitoka chumbani na kuja kumuita Seth na kumwambia kuwa Steven kaanguka.Kusikia hivyo Seth aliingia chumbani haraka na kumkuta kaka yake amelala chini hajitambui. Ndipo alipochomoka mbio kwenda kumuita daktari wake Kanumba.Aliporejea hakumkuta Lulu.

Dunia inataka kujua nini hasa kilitokea na masikio ya wengi yameelekezwa kwa Lulu ambaye kwa vyovyote vile anajua kilichotokea mule chumbani kwa kuwa yeye ndiye alikuwa na marehemu Kanumba chumbani kama wapenzi wakati balaa linapotokea.Lakini taarifa kutoka kituoni Oysterbay zinasema kwamba binti huyo mwenye umri wa miaka 18 amegoma kuongea chochote hadi awepo mwanasheria wake,na hata mwanasheria wake akifika ameomba arekodiwe kwenye kinasa sauti kila atakachoeleza kwa kuhofia ushahidi unaweza ukapindishwa baadae.Lulu bado yuko chini ya uangalizi mkali wa polisi.

Mwanasheria mmoja ambae amejitambulisha kwa jina la Revocatus Alexandria Jr. ameomba wadau na waandishi kusubiri taarifa za kidaktari kuhusu chanzo cha kifo cha Kanumba.Amesema amekuwa akifuatilia sakata hili tangu lilipoanza na kwamba hakuna uthibitisho kuwa Lulu alimsukuma marehemu,inawezekana Kanumba mwenyewe katika vuta nikuvute alipoteza balansi na kudondoka bila ya kusukumwa.

Amefafanua zaidi kwa kusema hata kama Lulu alimsukuma marehemu sio lazima chanzo cha kifo kiwe ni kusukumwa.Jingine amesema inawezekana vile vile Kanumba alikuwa na tatizo la moyo au msukumo wa damu na hivyo alipokasirika msumo wa damu ulibadilika,au labda moyo uliashindwa kufanya kazi inavyotakiwa ndio maana alianguka "Hata kama ni kweli alijigonga, subirini wathibitishe chanzo cha kifo ndipo tuendelee kujadili!. Najua msiba huu ni huzuni kubwa, lakini nawaombeni sana, lets not be judgemental kwa Lulu!. Mimi ni miongoni mwa waumini wakubwa wa the doctrine of "karma", kuwa there is nothing new under the sun, hakuna coincidence wala bahati mbaya, lolote ambalo limetokea, lilikuwa litokee tuu, yaani siku ya mpendwa wetu Kanumba ndio ilikuwa imefika, saa ilipotimia Mungu akamuita, hata asingesu kumwa, angefia usingizini!. Ni vizuri jamii tukafahamu si vema kuanza kuhukumu mtu kablaya preliminary investigation yoyote kufanyika

After all, there is life after life and life before life!, death ni change tu ya life form from physical body to spiritual body!.

Source: FASHION TAG

0 comments:

Post a Comment