Saturday, January 14, 2012

Regia Mtema afariki Dunia kwa ajali

Taarifa iliyoifikia hivi punde toka mkoani Pwani,zinaeleza kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Rejia Mtema amepata ajali mbaya sana mapema leo asubuhi katika eneo la Ruvu na kufariki dunia papo hapo wakati akiwa safarini kuelekea Mkoani Morogoro. 

Kwa Mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa mbunge huyo ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe gari lake amepinduka na gari hilo mara baada ya kumshinda wakati akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake katika eneo hilo la Ruvu.

Ndani ya Gari hilo kulikuwa kuna watu wengine wanne ambao bado hawajatambulika ni kina nani na wako kwenye hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani kwa Matibabu.

tutaendelea kujuzana zaidi kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia. 

Picha kwa hisani ya Michuzi.

0 comments:

Post a Comment