Saturday, September 17, 2011

Nafasi Ya Kazi Mjengwablog; Assistant Moderator/Editor

Mjengwablog ni blogu yako ya jamii shirikishwa inayohamasisha mijadala huru ya kijamii. Mwaka huu Mjengwablog inatimiza miaka mitano huku tukizidi  kupokea kazi  za wadau na maoni mengi ya watembeleaji yenye kuhitaji kupitiwa na moderator. Hivyo basi,  tumeamua kutangaza ajira ya assistant moderator atakayemsaidia ' Mwenyekiti' wa mijadala kwenye kazi  ya ku-moderate. Nafasi hii ya ajira ni ya ' full time'. Kituo cha kazi kitakuwa Dar es Salaam.

Majukumu:
1. Kupitia maoni ya wasomaji kabla hayajaingizwa jukwaani.
2. Kuendesha shughuli za kila siku za Mjengwablog ikiwamo kuratibu picha , habari  na taarifa mbalimbali zinazoletwa na wadau  ili zirushwe hewani.
3. Kutafuta na kuratibu shughuli za matangazo ambayo pia yatamwongezea mwombaji kipato kupitia kamisheni mbali na mshahara wake.



Sifa za mwombaji:
1. Awe na elimu ya kidato cha sita na kuendelea
2. Awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
3. Awe na uzoefu wa kazi husika ikiwamo kupiga picha na matumizi ya e-media.
4. Awe mbunifu na mwenye fikra hojaji ( Critical thinking and creativity)
5.  Awe ni mtu anayejituma
6.  Awe na utayari wa kujifunza na kuwafunza wengine.

Mwombaji akumbuke; Mjengwablog ni blogu inayokua na mlango wa kuingilia kwenye soko kubwa la ajira kwenye sekta ya new-media kwa siku za usoni.

Maombi yakiambatana na CV yatumwe kwa :
Au piga simu; 
 0712 95 61 31 / 0788 111 765/ 0754 678 252 
Siku ya mwisho ya kupokea maombi ni Septemba 30, 2011. 

0 comments:

Post a Comment