Thursday, April 14, 2016

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WIZARA YA AFYA - ZANZIBAR



TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI WIZARA YA AFYA - ZANZIBAR

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa kada mbali mbali katika Wizara ya Afya Unguja na Pemba kama ifuatavyo:-

1. AFISA TABIBU (CLINICAL OFFICER) 'Nafasi (1)'- UNGUJA na 'Nafasi' (1) – PEMBA.
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya 'Stashahahada ya Utabibu' kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.




2. WAUGUZI (NURSES) 'Nafasi (8)' UNGUJA na 'Nafasi (4)' PEMBA
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya 'Stashahada' katika fani ya Uuguzi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. FUNDI SANIFU MADAWA (PHARMACEUTICAL TECHNICIANS) 'Nafasi (2)' - UNGUJA 
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya 'Stashahada' katika fani ya Ufundi Sanifu wa Madawa kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. FUNDI SANIFU VIFAA, TIBA (BIOMEDICAL TECHNICIANS) 'Nafasi (3)' UNGUJA na 'Nafasi (1)' PEMBA
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari.
Awe amehitimu elimu ya 'Stashahada' katika fani ya Ufundi Sanifu Vifaa, Tiba kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. FUNDI SANIFU MAABARA (MEDICAL LAB. TECHNICIANS) 'Nafasi (1)' - UNGUJA
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari
Awe amehitimu elimu ya 'Stashahada' katika fani ya Ufundi Sanifu Maabara kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar


6. AFISA MAABARA TIBA (MEDICAL LAB. TECHNOLOGIST) 'Nafasi (1)' - UNGUJA
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari
Awe amehitimu elimu ya 'Shahada ya Kwanza' katika fani ya Maabara ya Tiba kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7. AFISA AFYA MAZINGIRA (ENVIRONMENTAL HEALTH OFFICER) 'Nafasi (2)' - PEMBA
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari
Awe amehitimu elimu ya 'Stashahada' katika fani ya Afya Mazingira kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

8. FUNDI VIATU (SHOES MAKER) 'Nafasi (1)' - UNGUJA
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari
Awe na Taaluma ya Ufundi wa Viatu vya Wagonjwa wa Viungo 

9. MPISHI (SHEFF) 'Nafasi (1)' - UNGUJA
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari
Awe amehitimu elimu ya 'Cheti' katika fani ya Upishi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

10. DOBI 'Nafasi (1)' - UNGUJA
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari
Awe amehitimu elimu ya 'Cheti' katika fani ya Ufuaji wa Nguo kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

11. KARANI TAKWIMU 'Nafasi (1)' - PEMBA
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari
Awe amehitimu elimu ya 'Cheti' katika fani ya Takwimu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


12. FUNDI UMEME 'Nafasi (1)' - PEMBA
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari
Awe amehitimu elimu ya 'Stashahada' au 'Cheti' katika fani ya Umeme kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

13. MTUNZA KUMBUKUMBU ZA AFYA (MEDICAL RECORDER) 'Nafasi (1)' - UNGUJA
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari
Awe amehitimu elimu ya 'Stashahada' au 'Cheti' katika fani ya Utunzaji Kumbukumbu za Tiba (Medical Record) kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

14. KATIBU MUHTASI 'Nafasi (1)' - PEMBA
Sifa za Muombaji:
Awe ni Mzanzibari
Awe amehitimu elimu ya 'Stashahada' katika fani ya Uhazili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jinsi ya Kuomba:
Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU, 
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 - ZANZIBAR.

Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao katika Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo 
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 15 Aprili, 2016 wakati wa saa za kazi.
Muombaji anatakiwa aiainishe nafasi ya kazi anayoiomba kati ya zilizotajwa hapo juu vinginevyo maombi yake hayatazingatiwa. 


0 comments:

Post a Comment