Thursday, March 10, 2016

KUITWA KWENYE USAILI - CALL FOR INTERVIEW - 3/10/2016



Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya
Ministries, Departments and Agencies and Local Government Authorities
(MDA's & LGA's), National College of Tourism (NCT), Institute of Judicial
Administration Lushoto (IJA), Tanzania Public Service College (TPSC),
National Food Reserves Authority (NFRA) na Weight and Measures
Agency (WMA), anatarajia kuendesha Usaili na hatimaye kuwapangia vituo
vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili.

Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia yafuatayo:
1. Usaili utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na
tarehe kama inavyoonesha katika nafasi husika.
2. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho cha
mkazi, kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
3. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne,
sita, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea
kutegemeana na sifa za mwombaji na mahitaji ya sifa kwa kada husika..
4. "Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo
za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
6. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
7. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyia usaili.
8. Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth
Certificate)
9. Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
10. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue
kuwa hawakukidhi vigezo, hivyo wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi
zitakapotangazwa.

ATTACHMENT TANGAZO 


0 comments:

Post a Comment