Friday, November 27, 2015

Mpokezi (Receptionist)



SEKRETARIATI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/H/90 20 Novemba, 2015

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 400 za kazi kama zilivyoorodheshwa katika tangazo hili

Mpokezi (Receptionist) – NAFASI 1

MAJUKUMU YA KAZI

• Kupokea wageni na kuwasaili shida zao.

• Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni wanaoingia ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.

• Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani.

• Kutunza na kudumisha usafi wa "Switchboard" na ofisi zake.

• Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma.

• Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani wanamiadi (Appointment) au wamepata idhni ya maafisa husika.

• Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa mbalimbali ofisini.

• Kupokea simu kutoka "Extension" za ndani na kupiga nje ya ofisi.

• Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa kwenda nje.

SIFA ZA MWOMBAJI

• Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati na kufuzu mafunzo ya Mapokezi na Upokeaji Simu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA

• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi


NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao ili wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vi. Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 4 Desemba, 2015
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kingereza.
APPLICATION INSTRUCTIONS:

xiv. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa
Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;

http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa 'Recruitment Portal')
xv. MUHIMU: KUMBUKA KUWEKA (ATTACH) BARUA YAKO YA MAOMBI. ANUANI YA BARUA HIYO IELEKEZWE KWA KATIBU, OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA S.L.P 63100 DAR ES SALAAM


Related Posts:

  • Senior Procurement Manager Job Title : Senior Procurement Manager Source : Reli Assets Holding Company Limited Requirements : Holder of professional qualifications, to a first degree level or equivalent in purchasing and supply management or supply… Read More
  • Program Officer- Business AdvisorJob Title : Program Officer- Business Advisor Source : CARE International in Tanzania Requirements : Bachelor degree in commerce, marketing, business administration or related field Job Description : Apply To :  Full Address… Read More
  • Financial Reporting ManagerJob Title : Financial Reporting Manager Source : The Guardian, July 5, 2011 Requirements : Bachelor's Degree in Accounting or equivalent Job Description :Managing the reporting requirements, processes and procedures for c… Read More
  • Driver Cum Office Assistants (7 Posts) Job Title : Driver Cum Office Assistants (7 Posts) Source : Public Service Pensions Fund Requirements : Holder of Form IV certificate and a valid Class "C" Driving License coupled with three years proven driving… Read More
  • Senior Supplies and Stores Officer Job Title : Senior Supplies and Stores Officer Source : Reli Assets Holding Company Limited Requirements : Holder of professional qualifications, to a first degree level or equivalent in purchasing and supply management o… Read More

0 comments:

Post a Comment