Thursday, March 19, 2015

KUJIUNGA NA JKT KWA KUJITOLEA MWAKA 2015


KUJIUNGA NA JKT KWA KUJITOLEA MWAKA 2015 TANGAZO KWA UMMA

MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) ANAWATANGAZIA VIJANA WOTE WA TANZANIA BARA NA VISIWANI WENYE SIFA ZA KUJIUNGA NA JKT KWA KUJITOLEA MWAKA 2015.

BARUA ZINAZOAINISHA SIFA ZA KIJANA KUJIUNGA NA JKT ZIMESHATUMWA MIKOANI AMBAPO MCHAKATO WA KUCHAGUA VIJANA MIKOANI NA WILAYANI NI KATI YA MWEZI MACHI NA APRILI 2015.

MUOMBAJI LAZIMA AWE MTANZANIA, MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 18 HADI 23 KWA WENYE ELIMU YA DARASA LA SABA HADI KIDATO CHA SITA, MIAKA 18 HADI 26 KWA WENYE STASHAHADA NA MIAKA 18 HADI 35 KWA WENYE SHAHADA NA KUENDELEA. PIA ASIWE AMEWAHI KUAJIRIWA NA CHOMBO CHOCHOTE CHA ULINZI NA USALAMA.

AIDHA, MUOMBAJI LAZIMA AWE NA CHETI CHA KUZALIWA, CHETI HALISI CHA KUMALIZA SHULE, CHETI HALISI CHA MATOKEO YA SHULE AU CHUO (ORIGINAL ACADEMIC CERTIFICATE/TRANSCRIPT).

INASISITIZWA KUWA NAFASI ZA JKT NI ZA KUJITOLEA NA ZINAPATIKANA MIKOANI NA SI MAKAO MAKUU YA JKT. WAZAZI, WALEZI NA VIJANA MNATAHADHARISHWA KUEPUKANA NA MATAPELI WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI WA FOMU BANDIA (TOA TAARIFA MAKAO MAKUU YA JKT UNAPOMUONA MTU WA AINA HIYO). AIDHA, YEYOTE ATAKAYE GUSHI VYETI AU KUJIPATIA NAFASI KWA NJIA YOYOTE YA UDANGANYIFU HATUA ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA

MAKAO MAKUU YA JKT



Related Posts:

  • Quality Improvement Advisors - 3 PostsJob Title : Quality Improvement Advisors - 3 Posts Source : The Guardian, June 30, 2011 Requirements : Experience in implementing newborn and child health programs, including … Read More
  • Marketing ExecutiveJob Title : Marketing Executive Source : The Guardian, June 30, 2011 Requirements : � UG - Any Graduate - Any Specialization � PG - Any PG Course - Any Specialization … Read More
  • Grants ManagerJob Title : Grants Manager Source : The Guardian, June 30, 2011 Requirements : The ideal candidate will have strong knowledge of USAID grants management policies and regulat… Read More
  • Administrative SpecialistJob Title : Administrative Specialist Source : The Guardian, June 30, 2011 Requirements : Candidates will have 2 or more years managing an office, preferably for USAID funded … Read More
  • Deputy Claims ManagerJob Title : Deputy Claims Manager Source : The Guardian, June 30, 2011 Requirements : � A university degree � An advanced diploma in insurance � At least 4 years working exper… Read More

0 comments:

Post a Comment