Sunday, January 4, 2015

TABIBU II (CLINICAL OFFICERS) – (NAFASI 7)



TABIBU II (CLINICAL OFFICERS) – (NAFASI 7)
22.0 TABIBU II (CLINICAL OFFICERS) – (NAFASI 7) Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto. Tabibu hawa watafanya kazi ya kutoa huduma ya kwanza na utabibu kwa wanachuo na jamii inayokizunguka chuo katika vyuo vya maendeleo ya Wananchi vilivyopo katika mikoa yote ya Tanzania Bara. 22.1 MAJUKUMU YA KAZI • Kazi zote zinazofanywa na Tabibu Msaidizi • Kutambua na kutibu magonjwa ya kawaida kwa wanachuo na jamii inayokizunguka chuo. • Kutoa ushauri wa kiafya kwa wanachuo na jamii inayokizunguka chuo. • Kusimamia utendaji wa watumishi walio chini yake na kufanya upasuaji mdogo • Kushiriki katika kupanga na kutekeleza huduma za Afya msingi • Kushauri na kuhamasisha wanachuo kuchangia huduma za afya na Mfuko wa Afya ya jamii. • Kufundisha somo la afya ya jamii chuoni. 22.2 SIFA ZA MWOMBAJI • Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita wenye Stashahada ya Tabibu ya miaka mwitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali. 22.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS B kwa mwezi.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i.       Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45

ii.       Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii.      Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv.       Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

v.       Waombaji  waambatishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza  (Detailed C.V)  yenye

anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

vi.    Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu


mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.

-       Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

-       Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

-       Computer Certificate

-       Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) 

-       Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma. 

vii.       Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. 

viii.       Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

ix.       Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

x.       Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi.       Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xii.       Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 18 Januari, 2015

xiii.      Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.

xiv.       Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.



Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika

Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,

Secretariat,
SLP.63100,

P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

Dar es Salaam.


0 comments:

Post a Comment