Sunday, January 4, 2015

(EDUCATION OFFICER GRADE II) –HISABATI (MATHEMATICS) (NAFASI 15)



(EDUCATION OFFICER GRADE II) –HISABATI (MATHEMATICS) (NAFASI 15)
13.0 AFISA ELIMU DARAJA LA II (EDUCATION OFFICER GRADE II) –HISABATI (MATHEMATICS) (NAFASI 15) Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto.Walimu hawa watafanya kazi ya kufundisha katika vyuo vya maendeleo ya jamii na Maendeleo ya Wananchi vilivyopo katika mikoa yote ya Tanzania Bara. 13.1 MAJUKUMU YA KAZI • Kufundisha somo la Hesabu katika vyuo 25 vya Maendeleo ya Wananchi vinavyofundisha mafunzo ya Ufundi Stadi. • Kuandaa maazimio ya kazi, maandalio ya masomo, zana za kufundishia /kujifunzia, mazoezi ya wanafunzi na majaribio. • Kutunga, kusimamia na kusahihisha mitihani kwa lengo la kutathmini maendeleo ya wanachuo. • Kuandaa mazoezi ya kazi kwa wanachuo na kusahihisha. • Kuandaa taarifa za kitaaluma na kutunza kumbukumbu za maendeleo ya wanachuo na kuwasilisha katika mamlaka husika. • Kufanya tafiti mbalimbali za kielimu. • Kushika zamu na kutoa taarifa kwa uongozi wa chuo. • Kutunza na kudhibiti matumizi ya vifaa katika sehemu aliyokabidhiwa. • Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa ngazi za juu kuhusu masuala mbalimbali kulingana na majukumu aliyopewa. • Kutoa ushauri nasaha na kuwalea wanachuo kwa kuwaandaa kiakili,kimwili,kitabia na kimwenendo ili waweze kujua wajibu wao kwa jamii • Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa Chuo 13.2 SIFA ZA MWOMBAJI • Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali waliosomea Hisabati na Ualimu (Bachelor of Education in Mathematics). • Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta 13.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGTS D kwa mwezi.

NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.

i.       Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45

ii.       Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii.      Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv.       Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.

v.       Waombaji  waambatishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza  (Detailed C.V)  yenye

anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

vi.    Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu


mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.

-       Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

-       Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

-       Computer Certificate

-       Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards) 

-       Picha moja "Passport size" ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma. 

vii.       Testmonials", "Provisional Results", "Statement of results", hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. 

viii.       Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).

ix.       Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

x.       Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.

xi.       Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xii.       Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 18 Januari, 2015

xiii.      Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.

xiv.       Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.



Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika

Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,

Secretariat,
SLP.63100,

P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

Dar es Salaam.


0 comments:

Post a Comment