Wednesday, January 28, 2015

Ajira Halmashauri ya Jiji la Tanga - Jan 2015



Ajira Halmashauri ya Jiji la Tanga - Jan 2015
Rejea mada hiyo hapo juu Kwa mujibu wa kibali cha Ajira mpya Kumb. Na. C8.170/369/01/96 cha tarehe 01 Decemba, 2014 tulichokipata tarehe 19/01/2015 toka kwa Katibu Mkuu Menejiment ya Utumishi wa Umma, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga anatangaza nafasi zifuatazo za Ajira kwa watanzania wote wenye sifa, na wenye umri wa miaka 18 hadi 45.

MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III TGS B.

SIFA ZA WAOMBAJI: .
Kwa mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Namba 1 wa mwaka 2013 kuhusu watendaji wa mitaa.
Waombaji wawe na Elimu ya kidato cha IV au VI,
waliohitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika mojawapo va fani zifuatazo:- Utawala, Sheria,
Elimu ya jamii (Sociology), Usimamizi wa Fedha (Financial Management), Maendeleo ya' jamii (Community Development) na Sayansi ya Sanaa (Social Work) kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo,. Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali

Mtendaji Wa Mtaa Daraja La II TGS C.

Waombaji wawe na Elimu ya kidato cha IV/VI
waliohitimu Stashahada katika. fani ya Uawala, Sheria, Elimu ya Jamii (Sociology), Usimamizi wa
Fedha (Finacial Management), Maendeleo ya Jamii (Community Development(, .na Sayansi ya Sanaa
(Social Work) kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.

Mkaguzi Wa Mji (Town/City Inspector)

SIFA ZA WAOMBAJI:
Waombaji wawe wamehitimu kidato cha sita.
Waombaji wawe wahitimu wa Shahada ya Sheria, Shahada va Utawala, usimamizi wa Fedha na Shahada ya Uchumi.

Fundi Sanifu Msaidizi Daraja La III Selemala

NGAZI YA MSHAHARA TGS A/B
Kwa mujibu wa Waraka wa maendeleo ya Utumishi
Namba 20 wa mwaka 2002, Nyongeza II: Kuhusu muundo wa Utumishi wa Mafundi Sanifu Technicians.

SIFA ZA WAOMBAJI:
Waombaji wawe wamehitimu kidato cha nne IV katika masomo ya Sayansi na ~ufuzu mafunzo ya
Ufundi katika fani ya Ufundi Seremala katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali au,
Waliomaliza kidato channe wenye Cheti cha majaribio ya Ufundi Seremala Hatua ya pili kutoka
Chuo cha Ufundi Seremala kinachotambuliwa na Serikali

Fundi Bomba Msaidizi Daraja III
NGAZI YA MSHAHARA TGS A/B
SIFA ZA WAOMBAJI:
Waombaji wawe wamemaliza kidato cha nne IV
katika masomo ya Sayansi na kufuzu mafunzo ya Ufundi katika fani ya Maji kutoka katika Chuo
kinachotambuliwa na Serikali au, Waliomaliza kidato cha nne wenve Cheti cha majaribio ya ufundi Bomba Hatua ya pili (Trade Test II) kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,

Fundi Msaidizi Daraja La II Umeme

NGAZI YA MSHAHARA TGS A/B

SIFA ZA WAOMBAJI:
Waombaji wawe wamemaliza kidato cha nne IV katika masomo ya Sayansi na kufuzu mafunzo ya Ufundi katika fani ya Umeme kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali au; Waliomaliza kidato cha nne wenye Cheti cha majaribio ya ufundi Umeme Hatua ya pili (Trade Test II) kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali.

Maafisa Maendeleo Ya Jamii Wasaidizi Daraja La III(x6) .

NGAZI YA MSHAHARA TGS B.

Kwa mujibu wa Waraka wa maendeleo ya Utumishi
Namba 7 wa mwaka 2002, na marekebisho yake ya tarehe 4 Agosti, 2008 katika Waraka Kumb. Na.
AC.62/260/01.

SIFA ZA WAOMBAJI:
Waombaji wawe wamehitimu kidato cha nne IV waliofuzu mafunzo ya cheti kwenye fani ya maendeleo ya jamii katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vya (Buhare, Rungemba) au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.

 Katibu Mahususi Daraja La III (x3)

SIFA ZA WAOMBAJI:
Kwa mujibu wa waraka wa maendeleo ya Utumishi Namba 9 wa mwaka 2002 nyongeza VI: Kuhusu muundo wa Utumishi wa Makatibu Mahususi
(a) Waombaji wawe wamehitimu kidato cha nne IV waliohudhuria mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu, wawe wamefaulu somo la Hati Mkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Computer kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata Cheti katika Program za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher

Msaidizi Wa Kumbukumbu Daraja La II(X3)
NGAZI YA MSHAHARA TGS B
SIFA ZA WAOMBAJI:
Kwa mujibu wa Waraka wa maendeleo ya Utumishi Namba 9 wa mwaka 2002 Nyongeza Namba V kuhusu muundo wa Utumishi wa Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II (Records Management Assistant II) Waombaji wawe wamehitimu kidato cha nne/sita wenye cheti cha Utunzaji wa Kumbukumbu katika moja wapo ya fani za Afya, Masjala na Ardhi.

KAZI YA AUXILIARY POLICE NAFASI ISHIRINI (20)

SIFA ZA WAOMBAJI:
WaombaJi wawe wamehitimu kidato cha nne waliohudhuria mafunzo ya:-
Auxiliary police kwa miezi isiyopungua sita toka Chuo cha Polisi Moshi.
Waliohitimu mafunzo ya JKT na kupata Cheti cha mafunzo ya JKT.
'Waliohitimu mafunzo ya mgambo na kupata cheti cha Mgambo.
Wawe wamefaulu angalau masomo matatu ya kidato cha nne.

APPLICATION INSTRUCTIONS:

Maombi yote yaambatane na vivuli vya vyeti vya masomo na mafunzo. -
Muda wa kuleta maombi ni ndani ya siku 21 kuanzia tarehe ya Tangazo hili, siku ya mwisho ya kupokea
maombi ni tarehe 16 Februari, 2015 saa 9.30 Alasiri.
Waombaji wote waweke namba zao za simu kwenye barua za maombi, majibuyatatolewa kwa njia ya
simu kwa wote watakaoitwa kwenye Usaili.
Waombaji wenye anuani za Barua Pepe (E-mail) na Fax waweke pia namba za simu katika barua zao
za rnaornbi, zitakazotumika kuwapatia majibu ya kuitwa kwenye usaili.
Waombaji waweke pia picha moja ya Passport Size iliyopigwa hivi karibuni katika barua zao za maombi
ya kazi.
Tuma kwa
MKURUGENZI
HALMASHAURI YA
S.L.P. 178
TANGA


0 comments:

Post a Comment