WALIOFAULU USAILI WA NAFASI 228 ZA
KONSTEBO NA KOPLO WA UHAMIAJI
KONSTEBO NA KOPLO WA UHAMIAJI
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliendesha usaili wa kujaza nafasi 228 za kazi ya Koplo na Konstebo wa Uhamiaji; ambao ulifanyika kuanzia tarehe 10 hadi 15
Novemba, 2014, katika kumbi za Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu (DUCE) Chang'ombe, Temeke, Dar es Salaam; na kuanzia tarehe 10 hadi 13 Novemba, 2014
katika ukumbi wa Ofisi ya Idara ya Uhamiaji uliopo Kilimani - Zanzibar. Baada ya usaili, uteuzi ulifanyika kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo: vipaumbele vya Idara
ya Uhamiaji, ufaulu kuanzia alama 50% na kuendelea, waliopitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa wenye alama za ufaulu pamoja na utaalam wa kuongea lugha za kigeni. Waliofaulu usaili wanatangaziwa kuripoti Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Mtaa wa Loliondo, Kurasini - Dar es Salaam, tarehe 1 Desemba, 2014, siku ya Jumatatu, saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya maelekezo zaidi. Aidha, wanatakiwa kwenda wakiwa na vyeti halisi vya masomo / mafunzo, cheti halisi cha kuzaliwa na picha mbili za rangi (passport size).
Tangazo hili limetolewa na:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
9 Barabara ya Ohio,
S. L. P 9223,
11483 DAR ES SALAAM
Waombaji wa kazi ambao majina yao hayamo kwenye orodha hii wafahamu kuwa hawakukidhi vigezo. Atakayeona tangazo hili amtaarifu na mwenzake. Tangazo hili linapatikana pia kwenye mbao za matangazo zilizopo kwenye Ofisi zote za Mikoa za Uhamiaji Tanzania.
Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
9 Barabara ya Ohio,
S. L. P 9223,
11483 DAR ES SALAAM
Waombaji wa kazi ambao majina yao hayamo kwenye orodha hii wafahamu kuwa hawakukidhi vigezo. Atakayeona tangazo hili amtaarifu na mwenzake. Tangazo hili linapatikana pia kwenye mbao za matangazo zilizopo kwenye Ofisi zote za Mikoa za Uhamiaji Tanzania.
***BONYEZA HAPO CHINI KUSOMA MAJINA YOTE ***
0 comments:
Post a Comment